WAANDISHI WA HABARI WAPATA SEMINA KUHUSU KILIMO CHA MAHINDI.
Mshauri mstaafu wa Jukwaa la
Bioteknolojia Tanzania (OFAM), Dk.Nicholas Nyange, akitoa mada kwa
waandishi wa habari kuhusu matumizi ya Bioteknolojia katika matumizi ya
kilimo walipotembelea kituo cha utafiti wa kilimo cha Makutupora mkoani
Dodoma.
Mshauri mstaafu wa mradi wa kuzalisha
mahindi yanayostahimili ukame kupitia mradi wa Wema, Dk. Alois Kullaya
akitoa mada kuhusu mahindi hayo yanayotokana na teknolojia uhandisi jeni
(GMO) kuhusu mafanikio ya mradi huo na changamoto zake.
Wanahabari wakiwa nje ya lango kuu la
kuingia katika shamba la majaribio la mahindi yaliyotokana na teknolojia
ya GMO la Makutupora mkoani Dodoma wakisubiri taratibu za kuingia
kwenye shamba hilo.
Mtafiti Ismail Ngolinda wa Kituo hicho
(kushoto), akitoa maelekezo kwa wanahabari kabla ya kuingia katika
shamba hilo la majaribio.
Mtafiti Ismail Ngolinda akiwaonesha wanahabari mahindi yaliyooteshwa kutokana na teknolojia hiyo ya GMO.
Wanahabari kutoka mikoa saba wakiwa katika picha ya pamoja na watafiti wa kilimo mbele ya shamba hilo.
Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com
Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com