UZURI WA MANDHARI ZA MLIMA KILIMANJARO UWAPO KILELENI.
Uoto wa asili wa aina mbalimbali unavyoonekana wakati unapoanza safari ya kuelekea kituo cha Kibo ukitokea kituo cha Horombo.
Mawe yenye michoro mithili ya mistari ya Pundamilia yanaonekana katika eneo lijulikanalo kama Zebra Rocks.
Kwa
mbali ni muonekano wa vibanda viwili maalumu kwa ajili ya kujisaidia
ambavyo viko njiani wakati unaelekea Kibo Hut ,eneo hili linajulikana
kama Last woter Point ni eneo la mwisho linaloonekana kuwa na maji.
Ndege
wakubwa aina ya Kunguru mwenye baka jeupe shingoni wanaonekana katika
maeneo haya wakisubiri mabaki ya chakula kutoka kwa wageni wanaopanda
Mlima Kilimanjaro.
Maeneo mengine yanaonekana kuwa na mabonde makubwa huku ukungu ukifunika uoto wa asili katika maeneo hayo.
Uoto
wa asili hupotea kabisa na kubaki nyasi fupi hasa maeneo ambayo
yamefunikwa na mchanga ,eneo hili ni maarufu kwa jina la Saddle .
Ukiwa
njiani katika eneo hili unapata nafasi ya kupita katikati ya vilele
viwili vya mlima Kilimanjaro yaani Kibo na Mawenzi na hiki ni kilele cha
Kibo ilipo Uhuru Peak.
Hii
ni sehemu tu ya vilima vilivyo njiani na eneo hili hutumika kwa ajili
ya kupata chakula kabla ya kuendelea na safari ya kuelekea Kibo Hut.
Ukipata bahati ya kuamka mapema ,hii ndio hali unayokutana nayo pindi uwapo katika safari ya kuelekea Kibo Hut.
Hii ni sehemu ya juu ya mlima ambayo hujulikana kama Jamaica ,sehemu ya mwisho kabla ya kufika Gilmans point.
Vilima vya barafu ni sehemu ya maumbile yanaoonekana katika eneo la jirani kabisa na kilele cha Uhuru.
Na
hapa ndio Kilele cha Uhuru ambako safari ya siku nne inakufikisha na
kuandika historia kuwa miongoni mwa watu waliowahi kufika eneo la juu
kabisa Afrika na la pili Duniani.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii ,Kanda ya Kaskazini.