SERA YA FILAMU KUWAKOMBOA WASANII WA FILAMU NCHINI TANZANIA.
Katibu Mtendaji, Bodi ya Filamu nchini Tanzania, Mama Joyce Fissoo.
Na BMGHabari
Bodi ya Filamu
nchini imebainisha kwamba kukamilika kwa sera ya kusimamia uendeshaji wa
tasnia ya filamu, kutasaidia kuwakomboa wanatasnia hiyo kwa kuinua
kuinua uchumi wao na wa Taifa kwa ujumla.
Katibu Mtendaji
wa Bodi hiyo, Bi.Joyce Fisso, aliyasema hayo jana wakati akihojiwa
kwenye kipindi cha Power Break Fast On Saturday kinachoendeshwa na
watangazaji Philip Mwihava na Godfrey Kusolwa.
"Kuwa na sera
ya filamu pia kutaongeza wigo wa uwekezaji kwenye tasnia hii, kutasaidia
kuondoa baadhi ya changamoto kwani bado taasisi za kifedha hazitambui
sekta hii ikizingatia kwamba mswada wa filamu ni kama mtaji hivyo lazima
sera iweze kutanabaisha wazi ili kuwasaidia wanatasnia kupata mikopo
kwa njia rahisi kupitia miswada". Amesema Fissoo.
Fissoo amesema
sera ya filamu itasaidia kuwezesha muono kwamba tasnia ya filamu ni
ajira, ni uchumi na inatoa fursa za kimaendeleo kwa wadau wake ambapo
bodi ya filamu inaendelea kupokea maoni ni namna gani sera hiyo iwe.
Pia Bi.Fissoo
aliwahamasisha watanzania kuzipigia kura filamu za Tanzania ili zishinde
tuzo za Africa Magic Viewer Choice za nchini Nigeria, akisema “Filamu
hizo
ni Naomba Niseme, Aisha na Home Coming ambazo zinawania tuzo za filamu
bora na
Siri ya Mtungi ambayo inagombea filamu bora ya lugha ya Kiswahili.
Niwaase
Wanzania, ushindi wa filamu hizi ni sisi kuwapigia kura hawa vijana wetu
ambao
wameshika bendera yetu kwenda kutuwakilisha kule Nigeria, niwasihi
waweze
kuzipigia kura na wahakikishe wanahamasisha marafiki zao pia kuzipigia
kura ili
nafasi zote tuzo zije Tanzania”.
Mtayarishaji wa
filamu nchini, Staphord Kihole (pichani) ambaye pia alikuwa kwenye
kipindi hicho, ametumia fursa hiyo kuwaomba watanzania kuzipigia kura
filamu za kitanzania ili zishinde tuzo za Africa Magic Viewers Choice
Awards zinazofanyika nchini Nigeria ikiwemo filamu yake ya "Naomba
Niseme" inayowania vipengele viwili, kikiwemo kipendele cha Best East
Africa na Best All Africa kinachoamuliwa na majaji.
Ili kuzipigia kura filamu za Tanzania
ambazo ni Naomba Niseme, Aisha na Home Coming, unapakua Application ya
We Chat, unajisajiri kwenye Africa Magic kwa kutumia nambari ya simu na
kisha unatafuta kipengele cha AMVCA na utaweza kupiga kura kadri
upendavyo ambapo mtu mmoja anaweza kupiga kura hadi 100 kwenye filamu
tofauti tofauti.