Rais Magufuli Ateua Mabalozi Watano Kuiwakilisha Tanzania nchi Mbalimbali na Pia Ateua Balozi Mmoja
Rais Magufuli Amteua Dkt.Abdallah Possi kuwa Balozi
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
Simu: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: press@ikulu.go.tz
Faksi: 255-22-2113425 |
OFISI YA RAIS,
IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Ikulu,
Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe
Magufuli, leo tarehe 19 Januari, 2017 amemteua Dkt. Abdallah Possi kuwa Balozi.
Kituo cha kazi na tarehe ya kuapishwa kwa Dkt. Abdallah
Possi itatangazwa baadaye.
Kabla ya uteuzi huo Dkt. Abdallah Possi alikuwa Naibu Waziri,
Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu aliyekuwa
akishughulikia Ulemavu.
Kufuatia uteuzi wa Dkt. Abdallah Possi kuwa Balozi, nafasi
ya Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na
Walemavu (Ulemavu) itajazwa baadaye.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
19 Januari, 2017