Picha: GARI LA KIFAHARI LA RAIS JAMMEH ALIYEKIMBIA NCHI BALAA..ANADAIWA KUKOMBA PESA KATIKA HAZINA YA NCHI YA GAMBIA
Yahya
Jammeh aliyeitawala Gambia kwa miaka 22, hatimaye jana aliondoka nchini
humo na kwenda kuishi uhamishoni baada ya kushindwa katika uchaguzi
mkuu wa Disemba Mosi mwaka jana.
Jammeh alishindwa na kiongozi aliyekuwa akiungwa mkono na vyama vya
upinzani, Adama Barrow ambaye amekuwa akiishi nchni Senegal alipoapishwa
kuwa Rais wa Gambia baada ya Jammeh kukataa kutoka madarakani awali.
Yahya Jammeh alipokuwa akiiongoza Gambia aliweza kujinunulia vitu vingi
vya kifahari na moja wapo ni gari lake la kifahari aina ya Rolls Royce.
Gari hili ambalo kwenye viti vyake ameandika jina lake, lina thamani ya
kati ya fedha za kitanzania milioni 500 hadi milioni 800. Rolls Royce ni
moja ya magari ya kifahari na ya kipekee duniani ambayo mara nyingi
hutumiwa na watu wenye uwezo mkubwa kifedha.
Gari hili la Yahya Jammeh liliwashangaza rais wengi wa Gambia lilipokuwa
likikatisha katika viunga vya mji wa Banjul kumpeleka kiongozi huyo
uwanja wa ndege tayari kuondoka nchini humo.
Licha ya kuwa Jammeh aliondoka nchini Gambia jana huku wananchi
wakishangilia kwa furaha, imeelezwa kuwa kiongozi huyo alikomba fedha
katika hazina ya nchini hiyo na kuiacha katika ukata mkubwa wa fedha.
Taarifa kutoka katika kambi ya Rais Adama Barrow zinaeleza kuwa dola za
kimarekani milioni 11 zilichukuliwa katika hazina ya nchi hiyo.
Yahya Jammeh tayari amewasili nchini Equatorial Guinea ambapo ndipo ataishi.
Hapa chini ni picha zaidi za gari hilo la kifahari;
Hapa ni sehemu ya magari ya Yahya Jammeh yaliyopo uwanja wa ndege wa
Banjul Gambia, baada ya ndege toka Guinea kuzuiliwa kuyachukua.