Picha 40: UZINDUZI WA WIKI YA MAADHIMISHO YA MIAKA 40 YA KUZALIWA KWA CCM..KONGAMANO LAFANYIKA SHINYANGA
Jumamosi Januari 28,2017-
Chama cha Mapinduzi wilaya ya Shinyanga Mjini katika mkoa wa Shinyanga
kimefanya Kongamano ikiwa ni uzinduzi wa wiki ya Maadhimisho ya miaka 40
tangu kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi CCM tarehe 05.02.1977.
Kongamano hilo limefanyika leo Katika Ukumbi wa CCM mkoa wa Shinyanga na
kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa wilaya ya Shinyanga mjini na mkoa
wa Shinyanga,makada wa CCM na vyama vya upinzani na watu mbalimbali
wenye mapenzi mema wakiwemo wanafunzi wa Shule ya sekondari Buluba na
Kom sekondari.
Mada mbalimbali zilitolewa wakati wa kongamano hilo ikiwemo historia ya
CCM na mafanikio ya chama hicho tangu kuanzishwa kwake mwaka 1977.
Katika kuadhimisha wiki ya maadhimisho ya miaka 40 ya CCM,Chama cha
Mapinduzi wilaya ya Shinyanga kitashiriki katika shughuli mbalimbali za
maendeleo katika ngazi ya matawi ikiwemo,kupanda miti,kusalimia
wagonjwa,watoto yatima,walemavu,kutembelea shule,michezo na kufanya
mikutano ya ndani badala ya mikutano ya hadhara.
Vyama asili vilivyozaa CCM ni Tanganyika African National Union (TANU)
cha Tanganyika na Afro Shiraz Party (ASP) cha Zanzibar vyote vikiwa ni
vyama vya ukombozi.
Kauli mbiu ya maadhimisho ya miaka 40 ya CCM ni "CCM Mpya,Tanzania Mpya".
Mwandishi Mkuu wa Malunde1 blog,Kadama
Malunde alikuwepo wakati wa Kongamano hilo,ametusogezea picha 40 za
matukio yaliyojiri ukumbini
Viongozi mbalimbali wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini na mkoa wa
Shinyanga wakiwa meza kuu.Wa kwanza kushoto ni Katibu wa CCM wilaya ya
Shinyanga mjini Charles Sangura,akifuatiwa na naibu meya wa manispaa ya
Shinyanga Agnes Machiya,Katibu wa CCM mkoa wa Shinyanga Alhaj Saad
Kusilawe,mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini Kanali mstaafu
Tajiri Maulid na meya mstaafu wa manispaa ya Shinyanga ambaye sasa ni
diwani wa Kata ya Kambarage Hassan Mwendapole
Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini Charles Sangura akizungumza
wakati wa kongamano hilo ambapo alisema katika kusherehekea miaka 40 ya
CCM watashiriki katika shughuli mbalimbali za maendeleo sambamba na
kufanya mikutano ya ndani badala ya mikutano ya hadhara
Makada wa CCM na wazee wa CCM wakiwa ukumbini
Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini Charles Sangura alisema lengo la
maadhimisho miaka 40 ya CCM ni kujimbusha walipotoka,walipo na
wanapoelekea.Kushoto ni Katibu mwenezi wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini
Rajab Makuburi
Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini Charles Sangura akizungumza ukumbini
Wanachama wa CCM wakiwa ukumbini
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini Kanali mstaafu Tajiri Maulid
akifungua kongamano hilo ambapo aliwataka wanaCCM kujivunia mafanikio
ambayo yamepatikana tangu chama hicho kianzishwe mwaka 1977
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini Kanali mstaafu Tajiri Maulid akisitiza jambo ukumbini
Wanachama wa CCM wakiwa ukumbini
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini Kanali mstaafu Tajiri Maulid
akizungumza wakati wa kongamano hilo ambapo aliwasisitiza wanachama wa
chama hicho pamoja na watanzania kwa ujumla kuendeleza mshikamano uliopo
nchini
Wanafunzi wa shule ya sekondari KOM wakiwa na mwalimu wao ukumbini wakifuatilia kilichokuwa kinajiri ukumbini
Viongozi mbalimbali wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini wakiwa ukumbini
Wafuasi wa CCM wakiwa ukumbini
Tunafuatilia kinachoendelea ukumbini
Mwalimu Patrick Kija alitoa mada kuhusu historia ya Chama Cha Mapinduzi na kuelezea harakati za ukombozi kutoka enzi za ukoloni
Mwalimu Patrick Kija akitoa historia ya CCM
Tunamfuatilia mtoa mada...
Aliyekuwa katibu tawala wa CCM mkoa wa Shinyanga Abdul Dachi akichangia mada kuhusu historia ya Chama Cha Mapinduzi
Katibu wa CCM mkoa wa Shinyanga Alhaj Saad Kusilawe akitoa mada kuhusu
mafanikio ya CCM tangu kianzishwe mpaka sasa.Alisema hata Muungano wa
Tanganyika na Zanzibar umeimarika zaidi
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini Kanali mstaafu Tajiri
Maulid,mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Erasto Kwilasa na diwani wa
kata ya Kambarage Hassan Mwendapole wakifuatilia kwa umakini kilichokuwa
kinaendelea ukumbini
Katibu wa CCM mkoa wa Shinyanga Alhaj Saad Kusilawe alisema chama hicho
kimeleta mabadiliko makubwa katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu,afya
,uchumi n.k
Tunafuatilia kinachoendelea
Meya mstaafu wa manispaa ya Shinyanga ambaye sasa ni diwani wa Kata ya
Kambarage Hassan Mwendapole akionesha ilani ya uchaguzi ya 2015 ya CCM
wakati akitoa mada kuhusu mafanikio ya CCM katika awamu ya tano
inayoongozwa na rais John Pombe Magufuli.
Mwendapole aliwataka wananchi kuwapuuza baadhi ya watu wanaobeza mafanikio yaliyofikiwa na CCM
Wanachama wa CCM wakiwa ukumbini
Makada wa CCM na baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani wakiwa ukumbini
Tunafuatilia kinachoendelea....
Mwanachama wa CCM Joseph Maige akichangia hoja ukumbini
Viongozi wa CCM wakifuatilia michango ya washiriki wa kongamano hilo
Kada wa CCM Charles Gishuli akichangia mada ukumbini
Mkuu wa wilaya mstaafu Zipporah Pangani akichangia hoja wakati wa
kongamano hilo ambapo aliomba Chama Cha Mapinduzi kijikite katika kutoa
elimu juu ya ilani ya uchaguzi ya chama hicho sambamba na kuimarisha
chama katika ngazi ya matawi
Mwanafunzi Mariam Mrisho anayesoma kidato cha tano katika shule ya
sekondari Buluba iliyopo mjini Shinyanga akichangia hoja katika
kongamano hilo
Kada wa CCM Mussa Jonas akichangia hoja ambapo alisisitiza umuhimu wa Chama Kujulikana kwanza badala ya mtu kujulikana zaidi
Mwanafunzi Stephen William kutoka Kom sekondari akizungumza ukumbini
Vijana wa CCM wakipiga makofi baada ya kufurahia jambo ukumbini
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Kanali Mstaafu Tajiri Maulid
akizungumza wakati wa kongamano hilo ambapo alisema katika kusherehea
miaka 40 ya CCM wamejipanga kushiriki katika shughuli mbalimbali za
maendeleo
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini akizungumza ukumbini
Mwenyekiti wa CCM mko wa Shinyanga Erasto Kwilasa akifunga kongamano
hilo ambapo aliwasititiza wanachama wa CCM kutoendekeza makundi ndani ya
chama
Kwilasa alisema pia alitumia fursa hiyo kuipongeza serikali ya awamu ya
tano inayoongozwa na rais John Pombe Magufuli kwa kujali wanyonge na
kuahidi kuwa chama hicho kitaendelea kuunga mkono jitihada zinazofanywa
na rais Maguful katika kurudisha heshima ya nchi
Vijana wa CCM wakiondoka ukumbini
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog