MWANDISHI WA HABARI KAMPUNI YA MWANANCHI COMMUNICATION ATOA MSAADA WA VIFAA VYA SHULE KWA BINTI SHULE YA SEKONDARI SIRARI.
MWANDISHI AKITETA JAMBO NA DIWANI WA KATA YA SIRARI PAUL NYANGOKO. |
DIWANI WA KATA YA SIRARI PAUL NYANGOKO AKIKABIDHI BEGI HILO KWA NIABA YA MWANDISHI WA HABARI LENGO NI KUSAIDIA BINTI HUYO AMBAYE AMENYIMA MAHITAJI YA SHULE BAADA YA KUKATAA KUKEKETWA. |
Akikabidhi
vifaa hivyo mwandishi wa kampuni ya Mwananchi Communication Waitara Meng’anyi
amesema kuwa ameamua kufanya hivyo baada ya kwenda kufanya mahojiano na binti
huyo na kubaini kuwa wazazi wake wameshindwa kununua vifaa vya shule ili kuendelea na masomo huku wakilazimisha binti
huyo kukeketwa na kuguswa na jambo hilo
hivyo amejitolea kutoa msaada huo.
“Sisi
waandishi wa habari siyo kwamba jukumu letu ni kuandika habari tu wakati
mwingine tunapaswa kusaidia jamii inayotuzunguka ili iweze kutimiza ndoto zake
nimeamua kusaidia binti huyu baada ya kunisimulia kisa chake na kuguswa”
alisema Waitara.
Aidha
Mwandishi huyo ametoa msaada wa Begi Moja na shilingi Elfu3,000 kwa ajili ya
kushona sare za Shule na kununua mahitaji mhimu ya shule.
Akikabidhi
kwa niaba ya Mwandishi huyo Diwani wa kata ya Sirari Paul Nyangoko amezidi kuwaasa
wazazi na walezi kuondokana na vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Binti Huyo
ambaye hakutaka jina lake kutajwa mwanafunzi wa kitado cha pili shule ya
sekondari Sirari amesema kuwa tangu apelekwe kidato ch kwanza mzazi maybe ni
baba wake wa kambo hajawai kununua sare za shule mpaka sasa huku akishikilia
madaftari mikononi.
Wazazi wangu
hasa mama mazazi amekuwa akinilazimishwa kukeketwa sasa imekataa na nilivyoenda
kutoa taarifa kwa mwenyekiti wa kijiji Baba, Mama na kaka walinipiga na
kuniumiza sana huku kaka akinitishia maisha naomba serikali inisaidia alisema
Binti huyo.