MVUA YA DAKIKA 10 YAZUA BALAA SHINYANGA USIKU HUU,NYUMBA ZAIDI YA 20 ZAEZULIWA NA UPEPO MKALI



Hapa ni katika shule ya MsingiViwandani iliyopo katika manispaa ya Shinyanga

Nyumba zaidi ya 20 zimeezuliwa na upepo mkali wakati mvua ikinyesha usiku huu wa Januari 11,2017 katika manispaa ya Shinyanga.

Inaelezwa kuwa kuna taarifa ya vifo ingawa mamlaka husika hajitoa taarifa kuhusu tukio hilo,tutawajuza pindi tu tukipata taarifa za uhakika.

Vyanzo vya habari vya Malunde1 blog vinasema mvua hiyo ya iliyoambatana na upepo pia imejeruhi watu kadhaa katika kata ya Kitangiri manispaa ya Shinyanga.

Diwani wa viti maalum tarafa ya Ibadakuli katika manispaa ya Shinyanga Zuhura Waziri (CCM) amefika katika baadhi ya maeneo yaliyoathiriwa na kujionea uharibifu uliojitokeza kufuatia mvua hiyo inayodaiwa kunyesha kwa muda takribani dakika 10 tu majira ya saa tatu usiku wa Jumatano Januari 11,2017.
Diwani huyo amesema  mvua hiyo mbali na kuharibu nyumba zaidi ya 20 pia madarasa manne na ofisi ya walimu katika shule ya msingi Viwandani zimeezuliwa.

Amewaomba wasamaria wema kufika katika eneo hilo ili kutoa msaada kwa wananchi waliothirika na mvua hiyo.
Jeshi la zimamoto limefanya jitihada za kuokoa mali mbalimbali
Taarifa kamili tutawaletea hivi punde
Powered by Blogger.