Mtoto amuua baba yake sababu ya asali
Jeshi la polisi linamtafuta mkazi wa
kijiji cha Kitenga Walayani hapa mkoani Mara Bakari Bakari (32) kwa
tuhuma za kumpiga baba yake mzazi kichwani kwa kitu chenye ncha kali na
kumsaabishia mauti.
Kamanda wa mkoa wa kipolisi Tarime
/Rorya Andrew Satta amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kumtaa aliyeuawa
kuwa ni Shaban Ramadhan (56) aliyefariki dunia baada ya kumkuta kiana wake
akiiba asali yake kwenye stoo.
Satta alisema kuwa tukio hilo
lilitokea katika kijiji cha kitenga januari 11 saa 4:00 usiku wakati marehemu
Shaban ambaye ni mfanyabiashara wa asali alipofungua mlango wa stoo yake kwa
lengo la kutunza mabaki ya asali.
Wakati akiingia ndani kijana wake
aliyekuwa ameishaingia ndani ya chumba hicho kwa nia ya kutaka kuiba asali
alimvamia baba yake na kumpiga kichwani kwa kitu chenye ncha kali na
kumsababishia mauti hapo hapo.
Mhudumu wa chumba cha kuhifadhia
maiti katika hospitali ya mji wa Tarime, Samwel Marindi alisema majira ya saa
4:00 usiku juzi alipigiwa simu na polisi wakimtaka afike katika eneo lake la
kazi kupokea mwili wa marehemu ambao umehidhiwa kwenye chumba hicho.
Shuhuda wa tukio hilo Alex Chacha
alisema walisikia yowe ikipigwa wakatoka nyumbani kuwenda kusaidia ndipo
walimkuta mwili wa marehemu ukiwa kwenye chumba alichokuwa kikitumia kama stoo
ya kuhifadhia asali na kupiga simu kituo cha polisi Sirari.
“Polisi walikuja wakafanya uchunguzi
na wakauchukuwa mwili kuupeleka Bomani ulipotunzwa, chanzo kijana alikuwa
nataka kuiba asali ya baba yake,” alisema Chacha.
Chacha ambaye ni Mwenyekiti wa
kitongoji cha Buriba Kata ya Sirari alisema kuwa marehemu nakusanya asali na
kuisambaza kwa wanunuzi wilayani Tarime na nje ya Tarime.
“Hatujajua kwa nini aliamua
kumsahambulia baba yake hadi kumsababishia mauti, kwangu hii ni familia
marafiki umekuwa msiba mkubwa,” alisema Chacha.
Hili ni tukio la aina yake kutokea
katika mji wa Sirari baada ya lile la desemba 29 mwaka Tajiri Robert
Mwikwabe alipompiga Risasi kwenye paji la uso Maite Amilly (17)
mwanafunzi wa kidato cha tatu katika sekondari ya Sirari na kufariki dunia hapo
hapo wakati wakigombea pumba za Mchele.
Mwisho.