MAKAMU WA RAIS MAMA SAMIA MGENI RASMI MAADHIMISHO YA MWAKA MPYA WA KICHINA.
Mkuu wa Kituo cha
Utamaduni wa China nchini Tanzania Gao Wei akizungumza na waandishi wa habari
(hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam kuhusu maadhimisho ya mwaka mpya wa
Kichina unaotarajiwa kuadhimishwa tarehe 21 na 22 mwezi huu katika viwanja vya Mnazi
Mmoja jijini Dar es Salaam. Maadhimisho hayo yataambatana na maonyesho ya utamaduni
wa Kichina. Kushoto ni Meneja Uhusiano wa Kampuni ya HUAWEI Jimmy Liguo Jin na
kulia ni Ofisa wa Ubalozi wa China, LIU Yun.
|
Na: Daudi
Manongi
Makamu wa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Hassan Suluhu anatarajiwa kuwa
mgeni rasmi katika maadhimisho ya mwaka mpya wa kichina yatakayofanyika katika
viwanja vya Mnazi Mmoja tarehe 21 na 22 January 2017 kuanzia saa tatu asubuhi
mpaka saa 11 Jioni.
Hayo yamesemwa
leo jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Kituo cha Utamaduni wa China nchini Bw.Gao
Wei alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari.
Amesema mwaka
huu utafahamika kama mwaka wa Jogoo wenye kuweka mtazamo mkubwa Afrika huku
yakiambatana na burudani nyingi kutoka kwa vikundi mbalimbali vya sanaa kutoka
China na nchini,maonyesho ya picha,vyakula vya kichina na maonyesho mbalimbali
ya kibiashara.
Katika
maadhimisho hayo makampuni 60 yatashiriki katika kuonyesha bidhaa
mbalimbali,pia nchi 150 na majiji 400 yatasherehekea maadhimisho haya ya mwaka
mpya.
Akizungumzia
mahudhurio ya siku hiyo Bw.Wei amesema kuwa wanategemea ushiriki wa watu zaidi
ya 6000 katika maadhimisho hayo ya siku mbili ambayo yanasisitiza zaidi urafiki
na mshikamano.
Katika
kufanikisha maadhimisho hayo Kampuni za HUAWEI na CRDB Benki zimejitokeza
kudhamini maadhimisho ya mwaka huu.