JINSI WAFANYAKAZI BENKI YA POSTA TANZANIA TAWI LA MBEYA WALIVYOSHEREHRKEA SIKU YA MAPINDUZI ZANZIBAR.
Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya Posta
Tanzania Tawi la Mbeya wakishiriki zoezi la usafi katika kituo cha Afya
kiwanja Mpaka jijini Mbeya ikiwa ni sehemu ya kusherekea miaka 51 ya
Mapinduzi ya Zanzibar .
Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya Posta
Tanzania Tawi la Mbeya wakishiriki zoezi la usafi katika kituo cha Afya
kiwanja Mpaka jijini Mbeya ikiwa ni sehemu ya kusherekea miaka 53 ya
Mapinduzi ya Zanzibar ambapo pia wakabidhi vifaa vya usafi katika kituo
hicho cha Afya .
Zoezi la usafi likiendelea
Erick Mwaigomole Mfanyakazi Benki ya
Posta Tanzania Tawi la Mbeya akishiriki kikamilifu shughuli za usafi
katika kituo cha Afya Kiwanja Mpaka jijini Mbeya kama sehemu ya
kusherekea Miaka 53 ya Mapinduzi Zanzibar.
Zoezi la Usafi likiendelea...
Meneja Msaidizi Benki ya Posta Tanzania
Tawi la Mbeya Joseph Nzilla akizungumza na waandishi wa habari kuhusu
zoezi la usafi ambalo limehusisha wafanyakazi wote wa benki ya posta
tawi la mbeya kama sehemu ya kusherekea miaka 53 ya Mapinduzi Zanzibar
Leo January 12, 2017.
Picha baadhi wa wafanyakazi benki ya
Posta Tanzania Tawi la Mbeya ambao wameshiriki zoezi la usafi katika
kituo cha afya kiwanja mpaka jijini Mbeya ikiwa sehemu yao ya kusherekea
miaka 53 ya Mapinduzi Zanzibar.
Meneja Msaidizi Benki ya Posta Tanzania
tawi la Mbeya Joseph Nzilla akimkabidhi vifaa vya usafi mganga mfawidhi
kituo cha afya kiwanja Mpaka Stella Moses kama sehemu ya mchango wao
ili kuendeleza zoezi la usafi katika kituo hicho.
Wafanyakazi wa Benki ya Posta Tanzania
Tawi la Mbeya katika picha ya pamoja mara baada ya kushiriki zoezi la
usafi katika kituo cha Afya kiwanja Mpaka jijini Mbeya ikiwa sehemu ya
kusherekea sherehe za Miaka 53 ya mapinduzi Zanzibar.
Imeandaliwa na Emanuel Madafa