ILIVYOKUWA KWENYE MKESHA WA KITAIFA WA MWAKA MPYA 2017.
Naibu Spika wa Bunge, Dk.Tulia Akson,
akipeperusha bendera ya Taifa wakati wa mkesha mkubwa wa kitaifa wa dua
maalumu uliofanyika Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam usiku wa kuamkia
Januari Mosi 2017. Dk.Akson alimwakilisha Rais Dk.John Magufuli kwenye
mkesha huo ambaye alikuwa mgeni rasmi.
Naibu Spika wa
Bunge, Dk.Tulia Akson (katikati), Mratibu wa mkesha huo Askofu Godfrey
Malesi na Askofu Damas Kenasi (kulia), wakishiriki kuomba katika mkesha
huo.
Waimbaji wa Kwaya ya Mass ya Sinza jijini Dar es Salaam wakiimba nyimbo za kumsifu mungu.
Watoto waimbaji wa Kwaya ya Mass ya Sinza jijini Dar es Salaam wakifanya vitu vyao kwenye mkesha huo.
Waumini wakiwa wameinua mikono kwenye mkesha huo.
Maombi yakiendelea.
Wananchi wakisubiri kuupokea mwaka mpya wa 2017 katika uwanja huo.
Shamrashamra za kuupokea mwaka mpya.
Mwaka mpya wa 2017 ukipokelewa.
Wananchi wakiwa wamelala wakisubiri kuupokea mwaka mpya.
Na Dotto Mwaibale
NAIBU Spika wa Bunge Dk. Tulia Akson
amesema Tanzania mpya na yenye matokeo chanya kwa mwaka 2017 inawezekana
hivyo akamataka kila mmoja wetu kufanyakazi kwa bidii ili kuliletea
taifa maendeleo.
Dk.Akson aliyasema hayo kwa niaba ya
Rais Dk.John Magufuli wakati akihutubia kwenye mkesha mkubwa wa kitaifa
wa dua maalumu uliofanyika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam jana.
"Tanzania mpya na nchi mpya yenye matokeo chanya kwa mwaka 2017 inawezekana" alisema Akson
Akson alimwakilisha Rais Dk.John
Magufuli alikuwa mgeni rasmi kwenye mkesha huo mkubwa ulioandaliwa na
makanisa mbalimbali ya kiroho.
Akinukuu baadhi ya maneno kutoka
katika kitabu cha biblia cha Nyakati mungu ataiponya nchi iwapo kila mtu
atamuita kwa jina lake na kujinyenyekesha na kuomba na kuziacha njia
mbaya.
"Tukimuita mungu kwa jina lake na kujinyenyekesha kwa kuacha kutenda mambo mabaya mungu ataiponya nchi yetu" alisema Akson.
Mratibi wa mkesha huo Askofu Godfrey
Malesi alisema hivi sasa kila Januari Mosi mikoa 17 hapa nchini imekuwa
ikifanya mkesha huo ikiwepo na Zanzibar kwa ajili ya kuwaombea viongozi
wa nchi na taifa kwa ujumla.
"Mungu amekuwa akijibu maombi yetu
tangu tuanze kuomba kupitia mkesha huu tulipoanza jijini Dar es Salaam
mwaka 1997" alisema Malesi.
Alisema tangu wakati huo wamekuwa
wakiiombea nchi iwe na amani na kuondokana na ufisadi na kumpata Rais
atakayeifanya Tanzania iwe mpya ambapo amepatikana Rais Dk.John Magufuli
ambaye ameifanya nchi kuwa na muelekeo mpya.
Alisema lengo lao ni kuhakikisha mkesha huo unafanyika katika mikoa yote na kila eneo la nchi yetu.
Mkesha huo uliopambwa na nyimbo
kutoka kwaya ya Mass ya Sinza jijini Dar es Salaam na Brass Band ya
Polisi ulihudhuriwa na viongozi wa dini kutoka nchi za jirani za Rwanda
na Burundi ambao walipata fursa ya kuzungumzia umuhimu wa nchi kuwa na
amani.