GLOBAL PEACE FOUNDATION WAHIMIZA AMANI KWA VIJANA MKOANI KAGERA.
Mwakilishi wa GPF Mkoani Kagera Bw. Benson Daud akizungumza na vijana katika Kongamano hilo.
Mtandao wa Blog za Mikoa
Mtandao wa Blog za Mikoa
Baadhi ya wanafunzi wakiwa wakimsikiliza kwa makini Bw. Benson (hayupo pichani) wakati wa Kongamano hilo
Baadhi ya wanafunzi kutoka shule mbalimbali wilayani Muleba wakimsikiliza kwa makini Diwani wa kata ya Bureza Bw.Deores Msinde(hayupo pichani)
Picha ya pamoja
Zaidi ya Vijana
150 kutoka Shule ya Sekondari Bureza, Shule za Msingi za
Butembo,Higabilo,Kinovelu wakiwa pamoja na Diwani wa Kata ya Bureza na
walimu wilayani Muleba Mkoani Kagera kupitia Programu ya Vijana na
amani inayo endeshwa na Global Peace Foundation(GPF), wamekutana katika
kongamano ambalo lengo kubwa ni kuhamasisha na kudumisha amani kutoka
katika ngazi ya Familia na jamii kwa ujumla.
Akizungumza na
wanafunzi hao Mwakilishi wa GPF Mkoani Kagera Bw. Benson Daud alisema
kuwa waliamua kuwakutanisha vijana wenye umri kati ya miaka 13-21 kwa
kuwa hao ndio wapo katika kundi ambalo limeathirika zaidi na uvunjifu
wa amani.
Alieleza kuwa
katika kata ya Bureza kumekuwa na matatizo mengi yanayowakabili vijana
ikiwa ni pamoja na utoro wa shule ambapo wengi wao huenda katika ziwa
Victoria kwa ajili ya kuvua samaki na kujifunza tabia zisizo njema
ikiwemo kuvuta Bangi na vileo vinginevyo, Mimba za utotoni ambazo nyingi
husababishwa na madereva wa bodaboda ambao hupelekea migogoro mikubwa
baina yao na familia pamoja na familia zenyewe kuchangia uvunjifu wa
amani kwa sababu ya wazazi kuwakatalia watoto shule na kuwalazimisha
wafanye biashara baada ya masomo.
Benson
aliwasihi wazazi na vijana kuachana na hayo mambo na vitendo vya
uvunjifu wa amani kwani wakifanya hivyo kutakuwa na amani na wataishi
vizuri katika jamii inayowazunguka.
Nae Diwani wa
Kata ya Bureza Bw. Deores Msinde aliwahimiza vijana kuwa mfano wa kuigwa
katika kudumisha amani, aliyasema hayo kutokana na mambo yanayoendelea
katika kata hiyo ambapo vijana ndio wanakuwa mstari wa mbele kuvunja
amani, "Naomba nitoe mfano katika kata yetu kumekuwa na mgogoro wa ardhi
ambapo wakulima na wafugaji wamekuwa wakitaka sehemu moja kwa ajili ya
kilimo na ufugaji jambo ambalo limepelekea makundi hayo ambao ni vijana
kupigana kila wakati huku wazee wakiwa wamekaa pembeni" alisema Diwani
Deores na kuwaomba vijana waachane na mambo hayo na kuwa serikali
inafanya jitihada za kutatua mgogoro huo.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti vijana mbalimbali wamefurahishwa na programu hiyo
inayoendeshwa na GPF ya 'VIJANA NA AMANI' na kusema kuwa itawasaidia
hata kuwaelimisha wengine umuhimu wa kulinda amani.