|
MKUU WA WILAYA YA TARIME GLORIOUS LUOGA AKIONESHA WANACHI MOJA YA KADI YA BIMA YA AFYA ZILIZOTOLEWA KWA KAYA 100 NA DIWANI WA KATA YA NKENDE CCM DANIEL KOMOTE IKIWA NI MOJA YA KUTEKELEZA ILANI YA CHAMA CHAKE. |
|
MKUU WA WILAYA YA TARIME AKISAINI KATIKA KITABU CHA WAGENI. |
|
DIWANI WA KATA YA NKENDE CCM DANIEL KOMOTE AKIELEZA KWA MKUU WA WILAYA YA TARIME LUOGA JINSI UJUENZI WA MADARASA SHULE YA MSINGI MAGENA UNAVYOENDELEA. |
|
DIWANI WA KATA YA NKENDE CCM AKIELEZA UMHIMU WA KUJIUNGA NA MFUKO WA JAMII (CHF) BAADA YA KUKABIDHI KADI ZA CHF KWA KAYA 100 |
|
MTENDAJI WA KATA YA NKENDE MARWA KONDOKO AKISOMA TAARIFA YA KATA HIYO. |
|
AMINA IBRAHIMU MENEJA WA BIMA ZANZIBA AKIELEZA UMHIMU WA KUJIUNGA NA MFUKO WA BIMA YA AFYA YA JAMII. |
|
DIWANI WA VITI MAALUMU CCM SALMA ABUBAKHAR AKIONGEA NA WANACHI WA KATA YA NKENDE . |
|
MGANGA MKUU HOSPITALI YA HALMASHAURI YA MJI WA TARIME CALVIN MWASHA AKIONGEA NA WANANCHI NA KUSISITIZA SUALA ZIMA LA KUJIUNGA NA MFUKO WA BIMA YA AFYA UKIWEMO MFUKO WA (CHF) |
|
KATIBU TAWALA WILAYA YA TARIME JOHN MARWA AKIONGEA NA WANACHI WA KATA YA NKENDE. |
|
MKUUWA WILAYA YA TARIME LUOGA AKIKABIDHI KADI ZA BIMA YA AFYA (CHF) KWA WANUFAIKA WAKIWEMO WAZEE, WALEMAVU NA WATU WASIJIWEZA ILI WAWEZE KUTIBIWA VYEMA. |
|
MWENYEKITI WA MTAA WA SONGAMBELE CHADEMA PAMBA CHACHA AKIKABIDHIWA KADI KUMI KWA AJILI YA WANACHI WAKE BAADA YA DIWANI WA KATA YA NKKENDEDANIEL KOMOTE (CCM) KUJITOLEA KULIPIA KAYA HIZO MBALI NA KULIPIA KAYA 100 KATIKA KATA YAKE "ALISEMA KUWA AKIPITA KATIKA MKUTANO WA HADHARA ULIKUWA UNAFANYIKA MTAA SONGAMBELE KATA YA SABASABA ALIKUTA AGENDA YA KUJIUNGA NA MFUKO WA BIMA YA AFYA NA KUWIWA NDIPO ALIAMUA KUKATIA FAMILIA KUMI |
|
MMOJA WA WANACHI AKIONESHA KADI YA BIMA YA AFYA ALIYOPEWA |
Diwani
wa Kata ya Nkende Daniel Komote(CCM) ameziwezesha kaya 100 kujiunga na Mfuko wa
Afya ya Jamii(CHF) ambapo watu 600 kutoka kaya hizo wamenufaika wakiwemo Wazee
na Walemavu.
Diwani
huyo alisema kuwa ameamua kufanya hivyo kwa lengo la kutimiza ahadi ikiwa ni
pamoja na kutekeleza ilani ya chama chake.
“Nimetoa
Bima hizi kwa kaya 105 mpaka sasa lakini hata wakifikia 115 nitawalipia ili
waweze kupata huduma ya Afya kwa uhakika mwaka mzima” alisema Komote.
Mkuu
wa Wilaya ya Tarime Glorious Luoga amekabidhi kadi za CHF kwa familia hizo zilizonufakika na msada huku na akiwataka
wanachi wengine kuiga mfano huo na kuweza kujiunga na mfuko wa Afya ya Jamii
Naye Mganga Mkuu Halmashauri ya Mji
wa Tarime Calvin Mwasha naye amezidi kuwasissitiza wanachi kujiunga na mifuko ya bima ya Afya huku
akisema kuwa suala la upumgufu wa madawa kwa sasa halitakuwepo kwani serikali
imejipanga vyema katika kuboresha huduma ya Afya.
Nao baadhi ya Wananchi ambao ni
wanufaika wameshukuru jitihada za diwani huyo
kwa kuwawezesha kujiunga na mifuko ya Bima ya Afya huku wakisii viongozi
wengine kuiga mfano huo.
PICHA ZOTE NA CLEO NEWSTZ KWA HABARI PIGA SIMU NO 0766424928