Shirikisho la
wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu Tanzania limetoa siku saba kwa
serikali kushughulia changamoto mbalimbali zinazowakabili wanafunzi
kuhusu mikopo.
Akizungumza na
wandishi wa habari Jijini dar es salaam katibu msaidizi wa shirikisho
hilo, Daniel Zenda amezitaja baadhi ya hujuma ambazo anadai zinafanywa
kwa makusudi na watendaji kutoka bodi ya mikopo ili kumkwamisha Rais
John Magufuli.
Aidha amesema
wanasikitishwa juu ya hujuma zinazoendelea kule bodi ya mikopo na
wamehuzunishwa kwa kiwango kikubwa baada ya sakata hili la mikopo
kuchukua taswira mpya ndani ya nchi, ambayo haipendezeshi sekta ya
elimu, kwa hiyo wamemejiridhisha kuwa kuna hujuma zinafanyika dhidi ya
serikali ili kumkwamisha Rais Magufuli.
"Miongozo
kutoka bodi ya ya mikopo na mwingine kutoka Wizara ya Elimu, hii
miongozo inakinzana, athari ya kupingana kwa hii miongozo inapelekea
wanafunzi wengi kukosa mikopo, kigezo cha umri hakipo katika miongozo
yote miwili lakini kule bodi ya mikopo kinatumika sisi tunaona ni hujuma
mojawapo," alisema
|