AJALI YA NOAH NA LORI ENEO LA TINDE MKOANI SHINYANGA YAACHA MAJONZI.
Na BMG, Kwa Msaada wa Mtandao
Watu 18 wamepoteza maisha na wengine wanne wakijeruhiwa katika ajali iliyohusisha gari aina ya Toyota Noah lililokuwa likitokea Nzega mkoani Tabora kuelekea Tinde mkoani Shinyanga lililogongana uso kwa uso na Lori Semi Teller katika Kijiji cha Nsalala Kata ya Tinde mkoani Shinyanga.
Kamanda wa polisi mkoani Shinyanga, Muliro Jumanne, amesema ajali hiyo imetokea jana majira ya saa moja jioni kwa kuhusisha Noah yenye nambari za usajili T 232 BQR iliyokuwa ikiendeshwa na Seif Mohamed pamoja na Lori Semi Teller lenye nambari za usajili T 198 CBQ lililokuwa likiendeshwa na Aloyce Kavishe.
Amesema miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya utambuzi na kwamba kwamba chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa Noah ambaye alitaka kuyapita magari mengine yaliyokuwa mbele yake bila kuchukua tahadhari ambapo madereva wote wanashikiliwa na polisi kwa ajili ya mahojiano na hatua za kisheria.