UN YAADHIMISHA MIAKA 71, YAAHIDI KUWEZESHA VIJANA.
Mgeni
rasmi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe.
Balozi Dkt. Augustine Mahiga (wa tatu kulia) akiwasili kwenye viwanja
vya Karimjee akiwa ameambatana na mwenyeji wake Mratibu Mkazi wa
Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo
(UNDP), Alvaro Rodriguez (wa pili kulia) pamoja na Mkurugenzi wa Idara
ya Ushirikiano wa Kimataifa wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa
Afrika Mashariki, Balozi Celestine Mushy (kushoto) kwenye sherehe ya
kupandisha bendera ya Umoja wa Mataifa katika kuadhimisha miaka 71 ya
umoja huo ambapo kila mwaka Oktoba 24 huadhimishwa.
Picha na Zainul Mzige
Picha na Zainul Mzige
WAKATI Umoja wa
Mataifa (UN) ukiadhimisha miaka 71 tangu kuanzishwa kwake, imeahidi
kuwatumia vijana katika utekelezaji wa malengo yake 17 ya maendeleo.
Mwakilishi
Mkazi wa UN nchini, Alvaro Rodriguez amesema ili kufanikisha hilo, UN
pamoja na mashirika mengine itatoa mafunzo ya vitendo kwa vijana zaidi
ya 50,000 ifikapo mwaka 2017 ambao wataingizwa katika mpango wa
utekelezaji wa malengo hayo.
"UN itaendelea
kushirikiana na vijana pia itatoa elimu ya vitendo.Hadi sasa vijana
zaidi ya elfu kumi wamepewa mafunzo na wanatambua malengo hayo, na
kwamba UN na wadau wengine wanatarajia kufundisha vijana zaidi ya 50,
000 ifikapo mwaka 2017, ili ifikapo 2030 vijana wengi wawe wanajua
malengo hayo na namna ya kuyatekeleza," amesema.
Amesema
miongoni mwa mafunzo yatakayotolewa kwa vijana hao ni pamoja na jinsi ya
kufanikisha malengo 17 ya maendeleo endelevu ya umoja huo na jinsi ya
vijana watakavyoweza kujiajiri.
Aidha,
Rodriguez amesema tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana linasababisha
umasikini kwa kuwa nguvu kazi hiyo inashindwa kuwajibika katika
kuliletea taifa maendeleo.
"Ongezeko la
vijana na mahitaji yao ni moja ya changamoto kubwa nchiniTanzania,
tunahitaji kuhakikisha kwamba vijana wanawajibika katika kujiendeleza
ili kupata maendeleo chanya katika maisha yao, ili kufanikisha hayo
vijana wanatakiwa kuwa na ufahamu na taaluma katika kuwezesha mabadiliko
ya uchumi nchini Tanzania," alisema Rodriguez na kuongeza: "Vijana
wasisahau kuwa wao ni chachu ya amani na maendeleo na UN tutaendelea
kushirikiana nao kuhakikisha vijana wanakuwa wadau wa taratibu na kanuni
zilizosababisha kuundwa umoja huu, wakijua na kutambua malengo ya
dunia," amesema.
Rodriguez amesema UN itaendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania katika kuleta maendeleo nchini.
Mgeni
rasmi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe.
Balozi Dkt. Augustine Mahiga akitambuliswa kwa Mwakilishi wa Shirika la
Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO)
nchini Afisa utawala na fedha, Spencer Bokosha (wa pili kulia) na
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika
la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez katika sherehe za maadhimisho ya
miaka 71 ya Umoja wa Mataifa tangu kuanzishwa zilizofanyika katika
viwanja vya Karimjee jana jijini Dar es Salaam.
"UN itashirikiana na serikali ya Tanzania kuleta maendeleo ikiwemo kuboresha utoaji wa huduma za kijamii," amesema.
Kwa upande wa
mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Balozi Augustine Mahiga amesema serikali inatambua mchango wa umoja huo
katika kuleta maendeleo nchini na kwamba itaendelea kushirikiana na
umoja huo.
"Serikali ya
awamu ya tano tangu kuanza kwake imefanya mambo mengi ili kuleta
maendeleo, imedhibiti mianya ya ukwepaji kodi, imefanikiwa kutanua wigo
wa ukusanyaji mapato na kuondoa rushwa. Hatuwezi kushinda pekee katika
kuleta maendeleo ya wananchi, serikali iko tayari kushirikiana na
jumuiya zote duniani," amesema.
Mgeni
rasmi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe.
Balozi Dkt. Augustine Mahiga akisalimiana na Mwakilishi wa Shirika la
Umoja wa Mataifa linalohudumia wakimbizi nchini (UNHCR), Chansa Kapaya
mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Karimjee kwenye sherehe ya
kupandisha bendera ya Umoja wa Mataifa katika kuadhimisha miaka 71 ya
umoja huo tangu kuanzishwa jana jijini Dar es Salaam.
Mgeni
rasmi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe.
Balozi Dkt. Augustine Mahiga akipokea heshima ya gwaride maalum kwenye
sherehe za kupandisha bendera ya Umoja wa Mataifa kuadhimisha miaka 71
ya umoja huo tangu kuanzishwa kwake zilizofanyika katika viwanja vya
Karimjee jana jijini Dar es Salaam.
Mgeni
rasmi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe.
Balozi Dkt. Augustine Mahiga akikagua gwaride la heshima lililoandaliwa
kwenye sherehe za maadhimisho ya miaka 71 ya Umoja wa Mataifa tangu
kuanzishwa kwake yaliyofanyika katika viwanja vya Karimjee jana jijini
Dar es Salaam.
Mgeni
rasmi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe.
Balozi Dkt. Augustine Mahiga akishuhudia kupandishwa kwa bendera ya
Umoja wa Mataifa ikiwa ni ishara ya maadhimisho ya miaka 71 ya umoja huo
tangu kuanzishwa kwake yaliyofanyika kwenye viwanja vya Karimjee jana
jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya wakurugenzi wa taasisi mbalimbali, serikali na wafanyakazi wa
mashirika ya Umoja wa Mataifa wakitoa heshima kwa wimbo wa Taifa wakati
wa kupandishwa kwa bendera ya Umoja wa Mataifa kwenye maadhimisho ya
miaka 71 ya umoja huo tangu kuanzishwa yaliyofanyika katika viwanja vya
Karimjee jana jijini Dar es Salaam.
Mgeni
rasmi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe.
Balozi Dkt. Augustine Mahiga akitoa hotuba kwenye sherehe za maadhimisho
ya miaka 71 ya Umoja wa Mataifa zilizofanyika katika viwanja vya
Karimjee jana jijini Dar es Salaam.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akimpongeza Mgeni rasmi Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt.
Augustine Mahiga kwa hotuba nzuri.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akitoa salamu za Umoja wa Mataifa
kwenye sherehe za maadhimisho ya miaka 71 ya Umoja huo tangu kuanzishwa
kwake zilizofanyika katika viwanja vya Karimjee jana jijini Dar es
Salaam.
Baadhi
ya mabalozi mbalimbali waliodhuria sherehe za maadhimisho ya miaka 71
ya Umoja wa Mataifa wakiwa jukwaa kuu katika viwanja vya Karimjee jana
jijini Dar es Salaam.
Meza
kuu, kutoka Kulia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mhandisi Hamad Masauni , Katibu Mkuu wa Asasi ya Umoja wa Tanzania
(UNA), Reynald Maeda, Brigadia Jenerali (TPDF), Dominic Mrope, Mgeni
rasmi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe.
Balozi Dkt. Augustine Mahiga, Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa
Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez
pamoja na Mkuu wa Mabalozi Balozi Prof. Ambrosio Lukoki.
Baadhi
ya wageni waalikwa wakiwemo wafanyakazi wa mashirika ya Umoja wa
Mataifa waliohudhuria sherehe za miaka 71 ya Umoja wa Mataifa
zinazofanyika Oktoba 24 kila mwaka ambapo jana zilifanyika kwenye
viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
Mshehereshaji
wa sherehe za maadhimisho ya miaka 71 ya Umoja wa Mataifa, Bertha
Makilagi (kushoto) akijadiliana jambo na Nguse Nyerere (kulia) Afisa
mwenzake wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika
viwanja vya Karimjee jana jijini Dar es Salaam.
Wanafunzi
wa shule msingi Uhuru Mchanganyiko wakitoa burudani wakati wa sherehe
za maadhimisho ya miaka 71 ya Umoja wa Mataifa yaliyofanyika jana katika
viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
Wanafunzi
wa Shule ya Sekondari Jitegemee wakitoa buradani katika sherehe za
miaka 71 ya Umoja wa Mataifa zilizofanyika jana jijini Dar es Salaam
katika viwanja vya Karimjee.
Mgeni
rasmi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe.
Balozi Dkt. Augustine Mahiga katika picha ya pamoja na waheshimiwa
mabalozi na viongozi mbalimbali huku wakiwa na mabango ya malengo ya
maendeleo endelevu (SDGs) katika sherehe za miaka 71 ya Umoja wa Mataifa
zilizofanyika kwenye viwanja vya Karimjee jana jijini Dar es Salaam.
Jukwaa
kuu katika picha ya pamoja na wanafunzi wa shule mbalimbali
waliohudhuria maadhimisho ya sherehe za miaka 71 ya Umoja wa Mataifa
yaliyofanyika kwenye viwanja vya Karimjee jana jijini Dar es Salaam.
Mgeni
rasmi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe.
Balozi Dkt. Augustine Mahiga (kulia) akibadilishana mawazo na Mkurugenzi
wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa wa Wizara ya Mambo ya Nje,
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Celestine Mushy (katikati)
wakati akijiandaa kuondoka kwenye viwanja vya Karimjee zilipofanyika
sherehe za miaka 71 ya Umoja wa Mataifa jana jijini Dar es Salaam.
Kushoto ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi
wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez.
Mgeni
rasmi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe.
Balozi Dkt. Augustine Mahiga akiagana na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya
Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro
Rodriguez baada ya kumalizika kwa sherehe za kupandisha bendera ya Umoja
wa Mataifa ikiwa ni maadhimisho ya miaka 71 ya umoja huo tangu
kuanzishwa kwake zilizofanyika katika viwanja vya Karimjee jana jijini
Dar es Salaam.
Mgeni
rasmi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe.
Balozi Dkt. Augustine Mahiga (kulia) akiteta jambo na Mratibu Mkazi wa
Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo
(UNDP), Alvaro Rodriguez wakati akijiandaa kuondoka kwenye viwanja vya
Karimjee jana jijini Dar es Salaam.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akizungumza jambo na mmoja wa wageni
waalikwa kwenye sherehe za kupandisha bendera ya Umoja wa Mataifa ikiwa
ni maadhimisho ya miaka 71 ya umoja huo tangu kuanzishwa kwake
zilizofanyika katika viwanja vya Karimjee jana jijini Dar es Salaam