MKUTANO MKUU WA WANACHAMA WA MUUNGANO WA KLABU ZA WAANDISHI WA HABARI NCHINI UTPC WAANZA JIJINI MWANZA.
|
Wajumbe wa
bodi, UTPC, wakiwa kwenye mkutano huo
|
|
Mweka Hazina
Mara Press Club akichangia jambo kwenye mkutano huo
|
|
Wajumbe
mbalimbali wakiwa kwenye Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Muungano wa Klabu za
Waandishi wa Habari nchini UTPC
|
|
Wajumbe
mbalimbali wakiwa kwenye Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Muungano wa Klabu za
Waandishi wa Habari nchini UTPC
|
|
Mwenyekiti
wa Mara Press Club, Mugini Jacob (kulia) akisalimiana na Rais wa UTPC, Deo
Nsokolo (kushoto) kwenye mkutano huo
|
|
Mwenyekiti
wa Mara Press Club, Mugini Jacob (kulia) akisalimiana na Makamu wa Rais wa
UTPC, Jane Mihanji (kushoto) kwenye mkutano huo
|
|
Mwenyekiti
wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoani Shinyanga, Kadama Malunde (kulia) akisalimiana
na Rais wa UTPC, Deo Nsokolo (kushoto).
|
Na
George Binagi-GB Pazzo
Waandishi wa Habari nchini wametakiwa kuusoma na kuuelewa vyema mswada sheria ya huduma ya vyombo vya habari 2016, uliowasilishwa na Serikali bungeni mjini Dodoma, kwa ajili ya kutoa maoni yao juu ya mswada huo.
Waandishi wa Habari nchini wametakiwa kuusoma na kuuelewa vyema mswada sheria ya huduma ya vyombo vya habari 2016, uliowasilishwa na Serikali bungeni mjini Dodoma, kwa ajili ya kutoa maoni yao juu ya mswada huo.
Rais
wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini UTPC, Deo Nsokolo, ameyasema
hayo kwenye Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Muungano huo, unaofanyika kwa siku
mbili Jijini Mwanza kuanzia leo.
Nsokolo
amesema tayari kamati ya bunge imekwisha kabidhiwa mswada huo kwa ajili ya
kukusanya maon hivyo ni vyema waandishi wa habari ambao wanaguswa moja kwa moja
na mswada huo, wakausoma kiundani na kisha kutoa maoni yao kabla ya
kuwasilishwa bungeni ili kuidhinishwa.
Akiwasilisha
mswada huo katika bunge lililopita, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo, Nape Nnauye, alisema ikiwa mswada huo utapitishwa na bunge kuwa
sheria, utasaidia kuleta mageuzi makubwa ya kitaaluma kwa wanahabari pamoja na
huduma za vyombo vya habari nchini.