KONGAMANO LA SAUTI YA MWANAMKE KUWAWEKA PAMOJA WANAWAKE JIJINI MWANZA KUJIFUNZA NA KUPATA BURUDANI.
Kongamano la Sauti ya Mwanamke ambalo
limeandaliwa na Kampuni ya CHOCOLATE PRINCES inayoandaa kipindi cha THE
MBONI SHOW chini ya mtangazaji wake Mboni Masimba, kinachoruka TBC1,
litawakutanisha wanawake wengi Jijini Mwanza kupata elimu ya kujikwamua
kiuchumi pamoja na kupata burudani.
Ni Jumapili tarehe 06.11.2016 katika
Ukumbi wa Gold Crest Hotel kuanzia majira ya saa kumi alasiri kwa
kiingilio cha shilingi elfu arobaini pamoja na chakula.
