NYUMBA 11 ZAUNGUA KWA MOTO TARIME.

BAADHI YA NYUMBA ZILIZOUNGUA MOTO HUKO NYAMONGO KATIKA KITONGOJI CHA NYABIKONDO KIJIJI KEWANJA WILAYANI TARIME MKOANI MARA


Kutokana na kutokea kwa matukio mbalimbali hapa nchini yaliyoibua sintofahamu kwa wananchi pamoja na serikali  nakuwaacha vinywa wazi kwa kuwasababishia hasara kubwa ikiwemo tetemeko la ardhi kutokea hivi karibuni  mkoani kagera na kusababisha maafa, makubwa katika kitongoji cha nyabikondo kijiji  cha kewanja Nyamongo Wilayani Tarime mkoani Mara  wakazi wa eneo hilo  wamejikuta wakikosa makazi na kulala nje  takribani siku tatu pamoja na mali zao baada ya nyumba zao za  nyasi  kumi na moja kuungua moto zenyewe kwa nyakati tofauti  na chanzo cha matukio hayo  kutojulikana kwani wananchi wamekuwa wakiona nyumba hizo zinawaka moto ghafla kwani tukio hilo  limeanza Septemba saba mpka septemba kumi huku baadhi wakidai kuwa ni ushirikina .

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wananchi hao   wakiwemo wahanga wa matukio hayo wamesikitishwa na hali hiyo huku wakibaki na sintofahamu ikiwa ni baada ya mkuu wa wilaya ya Tarime Gloriuos Luoga kufika maeneo hayo na kuzungumza na wananchi , viongozi wa serikali ,wazee wa milapamoja na  viongozi wa dini wakiwemo   na kusema kuwa serikali inaendelea na uchunguzi ili kubaini chanzo cha tukio hilo huku akiwasii kuwa waondokane na imani za kishirikina.

Akithibitisha kutokea kwa matukio hayo ya kuchomwa kwa nyumba hizo kumi na moja Mtanzania Omtima ambae ni mwenyekiti wa kijiji cha kewanja  amesema kuwa baada ya kutokea matukio hayo wamewza kufanya taratibu zote lakini mpaka sasa hata wao hawajabaini chanzo cha tukio hilo na kudai mpaka sasa hivi wananchi wake hawana makazi.
Hata hivyo wazee wa milia wamedai kuwa watakaa kwa ajili ya kuangalia suala hilo kwa kina huku wakiomba serikali kuendelea na uchunguzi juu ya tukio hilo.

Hali hiyo imempelekea mkuu wa wilaya ya Tarime Glorious Luoga  ambae ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama kufika maeneoambayo yamekumbwa na janga hilo  na kushuhudia nyumba hizo zilizo unguzwa kwa moto ambapo amewataka wananchi kuchukua tahadhari mapema kutokana na matukio hayo .

Hata hivyo  serikali wilayani Tarime kupitia halmashauri ya wilaya hiyo imeweza kutoa msaada kwa wahanga kiasi cha shilingi milioni mbili na laki mbili kwa kupatiwa wahanga kumi na moja wa nyumba hizo kiasi cha shilingi laki mbili huku mkuu wa wilaya akiongoza zoezi la kuchangia wahanga hao nakupatikana  shilingi laki tatu kwa ajili ya kupatiwa mahitaji kama chakula .
BAADHI YA NYUMBA ZILIZOUNGUA KWA MOTO.
MKUU WA WILAYA YA TARIME GLORIOUS LUOGA KULIA AKIONGEA NA MMOJA WA WAHANGA WA TUKIO LA KUUNGUA MOTO KWA NYUMBA KATIKATI NI MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA TARIME APOO CASTRO TINDWA




Powered by Blogger.