MTOTO NA MAMA WAPIGWA NA NYUNDO NA BABA MZAZI.
PICHA YA BHOKE WANKYO AKIWA AMESHIKILIWA NA BIBI YAKE ESTHER CHARLES KATIKA OFISI YA WASAIDIZI WA KISHERIA KATA YA NYARERO WILAYANI TARIME MKOANI MARA. |
Mtoto mmoja aliyejulikana
kwa jina la Bhoke Wankyo Mwita mwenye umri wa miaka 08 mkazi wa kitongoji
cha Nyankorambe kijiji cha Nyakungurui
kata ya kibasuka wilayani Tarime mkoani Mara amepigwa na nyundo na baba yake
mzazi aliyejulikana kwa jina la Mwita Wandwi mkazi wa kijiji cha Nyakunguru
kata ya kibasuka Wilayani Tarime mkoani Mara na kumusababishia maumivu makali
mtoto huyo.
Akiongea na
Jamboleo mtoto huyo aliyefanyiwa vitendo vya ukatili Bhoke Wankyo alisema kuwa
baba yake alimpiga kwa nyundo miguu yake miwili baada ya kuchelewa kutoka mtoni
akiwa na mama yake mzazi
“Tulipofika
nyumbani na mama baba alisema tumechelewa ndipo alianza kumpiga mama na badae
akaanza kunipiga mimi miguu kwa kutumia nyundo na miguu yangu imeumia sana
naomba serikali ichukue hatua kali na mama yangu akatibiwe” alisema mtoto.
Kwa upande
wake Esther Charles ambaye ni Bibi yake
na mtoto aliyefanyiwa vitendo vya ukatili amezidi kuomba serikali kuingilia
kati ili kunusuru maisha ya mtoto wake kwani mbali na kupigwa vikali mjukuu
wake bado mama yake na mtoto
anayejulikana kwa jina la Rhobi Wankyo ambaye pia ni mlemavu wa kutosikia na kuongea amepigwa vikali na mme wake na mpaka sasa
yuko nyumbani kwake na mpka sasa hajapata msaada wowote ili kuokoa maisha yake
na hapa mama yake mzazi ambaye ni bibi yake na mtoto huyo anaeleza.
Esther
alisema kuwa baada ya kupata taarifa hizo alifunga safari mpaka kwa mtoto wake
ili kushudia tukio hilo ndipo alikuta mtoto wake pamoja na mjukuu wake
wamefanyiwa vitendo vya ukatili lakini hakuna serikali ya kitongoji wala kijiji
na kata walikuwa wamefanyia kazi kuhusiana na tukio hilo huku wakimuzungusha
baada ya kuitaji msaada ili kusaidia mjukuu wake na ndipo alihamua kufika kata
jirani ya Nyarero kwa ajili ya kupata msaada wa kisheria ili kunusuru maisha ya
mtoto huyo ambaye miguu ilikuwa imeishaanza kuhoza.
“Nilipofika
hapa niliwaelezea wakanisaidia shilingi elfu kumi nikaenda kituo cha polisi
kupewa kibali cha kutibu mujukuu wangu na mpaka sasa nataka kwenda hospitai
lakini mwanangu bado yuko kwake hajapata matibabu yeyote” alisema Esther.
Hata hivyo
Esther alisema kuwa mbali na kupigwa kwa mjukuu wake bado mtoto wake ambaye ni
mama wa mtoto huyo ambaye pia ni mlemavu wa kutosikia na kuongea amepigwa
vikali na nyundoo mme wake na kumusababishia maumivu lakini mpka sasa hakuna
msaada wowote ambao amesaidiwa ili kunusuru maisha yahoo.
Naye diwani
wa kata ya Nyarero John Mhabasi
amezidi kulaani kitendo hicho
baada ya kuona kitendo cha kinyama alichofanyiwa mtoto huyo huku akihaidi kumusaidia mtoto
huyo ili apate matibabu kwa ajili ya kupona miguu yake ambayo amepigwa na
nyundo na baab yake mzazi
“Hata mimi
nachukua fursa hii kulaani kitendo hiki cha kinyama na kata yangu wananchi
wasijwe wakafanya unyama kama aliofanyiwa mtoto huyu” alisema Diwani kata ya
Nyarero.
Pia John
Sanyaro pamoja na Thomas Joseph ni wasaidizi wa kisheria kata ya Nyarero ambapo
amekimbia bibi wa mtoto huyoili kupata msaada wa kisheria wamezidi kulaani
vitendo vya ukatili huku wakiwaomba wenyeviti wa vitongoji, vijiji na watendaji
wa kata kuendelea kufuatilia vitendo vya ukatili vinavyofanywa na wazazi ili
kuwasaidia wanachi
“Jukumu la
ulinzi na usalama ngazi ya kitongoji ni la mwenyekiti wa kitongoji hawana budi
kuendelea kushilikiana vyema na wasaidizi wa kisheria pamoja na mshirika ambayo
yamejikita kupinga ukatili ili kukomesha ukatili wa kijinsia Tarime”
alisema sanyaro.
……..Mwisho….