KIBOYE CCM TUMEFURAHI KUPEWA RUNGU NA MAGUFULI.
PICHA YA MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI WILAYANI RORYA MKOANI MARA SAMWEL KIBOYE. |
Chama cha mapinduzi kupitia viongozi wake pamoja na wafuasi
wa chama hicho hapa nchini wamekuwa wakijivunia kwa kumpata rais anayetokana na
chama hicho kulingana na utendaji wake wa hapa kazi tu ukiwemo utumbuaji majipu suala ambalo
linasemwa na viongozi kuwa jambo hilo linaendelea kuleta sifa kubwa kwa chama
hicho na kubadili miendendo na tabaia za baadhi ya viongozi wavivu.
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi wilayani rorya Mkoani Mara
Samwel Kiboye akiongea na jambole
alisema kuwa amefurahishwa na kitendo cha rais wa jamhuri wa muungano wa
Tanzania Dk.John Magufuli kwa kuwapa rungu ya kuwasimamia watumishi wa umma na
kuwawajibisha watumishi waliochini yao pale wanapoenda tofauti na maadili yao
ya kazi.
Aidha kiboye huyo alisema kuwa katika kikao kilichofanyika
hivi karibuni Ikilulu jijijni Dar es salaam baada ya kukutana na Rais wa
jamhuri ya muungano wa Tanzania aliwambia kuwa wenyeviti hao hawana budi kusimamia vyema
ilani ya chama cha mapinduzi kwa lengo la kuwaletea watanzania wote maendeleo
bila kujali itikadi za vyama jambo ambalo litaendelea kukipa sifa chama hicho.
“Tayari magufuli ameisha tupa rungu hivyo ni jukumu letu
kufanya kazi kwa kushirikiana ili kuendana
na kasi ya rais wetu wa Nchi ambaye kwa sasa anapambana vikali bila kuangalia
mtu yeyote usoni huku” akisema hapa kazi tu kwa lengo la kuhakikisha anati miza
ahadi zilizotolewa kipindi cha kampeni” alisema.
Hata hivyo kiboye amewashauri viongozi wa vyama wa siasa bila kujali
itaikadi ya vyama vyao kwa lengo la kutekeleza ilani ya chama cha mapinduzi
baada ya kuchagua viongozi wanaotokana na chama hicho akiwemo rais pamoja na
madiwani na wabunge ambao ulifanyika oktoba 25 mwaka jana.
Kiboye alisema kuwa
magufuli amewapa rungu wenyeviti wa ccm wa mikoa na wilaya Nchi nzima baada ya kuitwa ikulu kwa kuwa
wasimamie watumishi waliko katika mfumo wa serikali na kuweza kutoa taarifa
katika mamlaka husika za uteuzi pale wanapokaidi kutekeleza ilani ya chama
hicho.
Kiboye alisema kuwa Rais Magufuli amewakutanisha ikulu wa
mikoa na wilaya Nchi Nzima na kuwapa maelekezo ya kuwasimamaia watumishi wote
kwa lengo la kuwaletea wanchi maendeleo kam a ilani ya chama cha mapinduzi
inavyosema kuwa chama hichi kitahakikisha kinatekeleza yale yanayosemwa na
ilani ya cam hicho kwa lengo la kuwaletea watanzania maendeleo.
“Hatutajali mtumishi yeyoye aidha anatokana na upinzani au
ccm kwa sababu wote wanajua ilani inayotekelezwa ni ya chama tawala hivyo kila mtu hana budi kuunga pia juhudi za
magufuli na tutawashangaa wale wanasema kuwa magufuli hatendei haki viongozi wa
umma wakati lengo lake ni kuhakikisha kila mtanzania wa chini nanufaika na keki
ya Taifa” alisema Samwel.
Mwenyekiti ameongeza kuwa kuwa wanchi wa wilaya ya Rorya wamekuwa wakipuuza suala zila kilimo na badae kukumbwa na janga la njaa suala ambalo kwa sasa hawana budi kulikemea ili wanachi waweze kulima kulingana na kauli ya Rais wa jamhuri ya muungano waTanzania ya hapa kazi tu.
“Vijana wengi wa rorya ni kuamkia kwenye vijiwe na kucheza puli wengine wanahamukia kwenye ziwa na kuendeleza unywaji wa pombe japo kwa sasa baa zote zimepigwa marufuku sasa kati ya maelekezo niliyopewa kutoka kwa rais wetu nyiemakatibu kata na tawi kuna haja kubwa ya kwenda kushirikiana na watendaji wa kata na vijiji ili kuhimiza wanchi wetu waweze kulima” alisema Mwenyekiti.
Hatam hivyo mkuu wa mkoa wa mara magesa mulungo ameweza kuagiza kuwa kila mwanchi wa mkoa hana budi kulima aidha zao la muhongo au mahindi heka mbilimbili kwa kila kaya na kuwaagiza wakuu wa wilaya huska kusimamia vyema suala hilo.
Akiongea katika kikao mkuu wa wilaya ya Rorya Felix Lyaniva alisema kuwa,Kutokana na agizo lililotolewa na mkuu wa mkoa wa Mara Magesa Mulongo kuhusu wanachi wa mkoa wa Mara kujikita katika suala la kilimo kwa kila kaya kuhakikisha inalima heka mbili kwa lengo la kuepukana na njaa Mkuu wa wilaya huyo amewataka watendaji wa kata , vijiji na maofisa ugavi kuanza kutekeleza amri alali ambayo alilitoa kwa ajili ya kutekeleza juu ya kilimo ili wilaya ya rorya kuondokana na suala la njaa.
Aidha Mkuu wa wilaya huyo alisema kuwa wanachi ambao watakikuka amri halaili hizo na kusindwa kulima wataenda kulima kwa lazima magereza kwa lazima kwani wilaya hiyo hataki kusikia sualazima la njaa
“Nilisha sema na kila siku nasema kuwa Rorya bila njaa inawezekana baada ya wanchi kujikita katika sula zima la kilimo na kuondokana na uzurulaji hovyo sasa makatibu kata na tawi ambao mko ndani ya kikao hiki hebu nendeni mkasaidiane na watendaji wangu wa serikali” alisema Mkuu wa Wilaya .
Hayo yamebanainishwa katika kikao cha Dharura Halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi wilayani Rorya Mkoani Mara kwa ajili ya kupokea maelekezo ambayo yalitolewa na Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi wilayani Rorya Mkoani Mara Samwel Kiboye.
Aidha katika kutoa maelekezo hayoMwenyekiti wa chama cha mapinduzi wilayani Rorya mkoani Mara amezidi kuongeza kuwa kuwa chamacha mapinduzi wilayani humo kitaendelea kumuunga mkono rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania katika suala zima la utumbuaji majipu.
Wakiongea wa nyakati tofauti wanachi wa wilaya ya Rorya Mkoani Mara kuhusu kilimo walisema kuwa kwa sasa kuna haja kubwa ya kuendelea na kujishughulisha na suala zima la kilimo cha mihogo ili kuweza kuondokana na suala zima la janga la njaa.
Aidha wanachi hao walisema kuwa serikali kupitia maofisa kilimo na hawana budi kuwaletea mbegu kinzani kwa ajili ya kuepukana na ugonjwa ambao umekuwa ukishambulia mihogo mashambani suala ambalo linawakatisha tama wanachi hao ambao wamejikita katika suala zima la kilimo.
“Sisi wananchi wa rorya tutajikita kwenye kilimo kama kauli ya rais wetu inavyosema kuwa hapa kazi tu ili tuweze kuzalisha chakula cha kutosha na ikiwzekana tuweze kulisha wilaya za jirani kama Tarime na Musom kwa ajili ya kuwa mfano” walisema Wanachi hao kwa Nyakati Tofauti.
Hata hivyo wanachi hao waliongeza kuwa serikali haina budi kuingilia kati ili kumaliza migogoro ya ardhi na kuwanyanganya wale walijimikilisha maeneo kwa muda mrefu na kutoyatumia ili wanchi waweze kulima.