HUDUMA YA X-RAY TARIME ZAANZA KUTOLEWA.

PICHA YA DR CALVIN MWASHA AKIONGEA NA WAANDISHI WA HABARI OFISINI KWAKE KUHUSU X-RAY KUFANYA KAZI.  
Hatimaye huduma za X-Ray zimeanza kutolewa katika Hospitali ya Wilaya ya Tarime baada ya juhudi a zinazofanywa na Mkuu wa Wilaya ya Tarime(DC) Glorius Luoga kuboresha huduma katika hospitali hiyo kuendelea kuzaa matunda.

Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji wa Tarime(DMO) Dr Calvin Mwasha amethibitisha leo kuwa tayari huduma za X-Ray zimeanza kutolewa hospitalini hapo baada ya huduma hizo kutokuwepo kwa takribani miaka miwili.

“ This is good news(hii ni habari njema) kwetu na kwa wakazi wa Tarime kwani sasa Machine yetu ya X-Ray inafanya kazi baada kufanyiwa matengenezo”, Dr Mwasha aliwaambia waandishi wa habari ofisini kwake leo mchana.

Ukosefu wa huduma za X-Ray katika hospitali hiyo umekuwa ukisababisha shida kubwa kwa wagonjwa.


Powered by Blogger.