DC TARIME APONGEA HALMASHAURI YA MJI KATIKA UKUSANYAJI WA MAPATO.

PICA YA MKUU WA WILAYA YA TARIME GLORIOUS LUOGA AKIONGEA JANA NA 
WAANDISHI WA HABARI OFISINI KWAKE.

 Mkuu wa wilaya ya Tarime Glorious Luoga ameipongeza Halmashauri ya mji wa Tarime kwa juhudi kubwa katika ukusanyaji wa mapato ambapo kwa mwezi mmoja tangu kuanza ukusanyaji wa tozo za majengo Halmashauri hiyo imekusanya zaidi ya shilingi 40,000,000 ambazo zinatokana na tozo hizo za majengo baada ya agizo la serilkali kuwa wanachi walipie tozo ya majengo kwa lengo la kuongeza mapato katika Halmashauri huska.


Luoga alisema kuwa pia anatumia fursa hiyo kuwashukura wanachi wa mji wa Tarime kwa mwitikio mkubwa huku akimupongeza mbunge wa jimbo la Tarime mjini Esther Matiko kwa ushirikiano ambao amekuwa akitoa katika suala zima la kukamilisha zoezi hilo.

Mkuu wa wilaya alisema hayo kipindi akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake jana huku akizidi kuwasaii wanachi hao kuendelea kulipa tozo hizo ili halmashauri ipate fedha za kutosha kwa lengo la kutekeleza miradi ya maendeleo ikiwemo uboreshaji wa sekta ya Afya , maji Elimu na Barabara.

“Mbunge wa jimbo la Tarime mjini Matiko nampongeza sana ameweza kuhamasisha wanchi wake na wameitikia kwa kiwango kikubwa na mpaka sasa Halmashauri ya mji Tangu kuwepo haijawahi kukusanya mapato zaidi ya millioni Nne kwa mwezi na ukiangalia Halmashauri ya mji haina vyanzo vya mapato vya kutosha” alisema Luoga.

Hata hivyo Mkuu wa wilaya huyo alisema kuwa mbali na Halmashauri ya vijijini madiwani akiwemo mbunge wa jimbo hilo John Heche kukataa tozo hizo kutozwa Luoga alisema kuwa bado amri hiyo hajaitoa na muda wowote itatolewa hivyo wanachi watatakiwa kulipa tozo hizo kwani ni jukumu la serikali kutekeleza sheria zinazazowekwa.

“ Halmashauri ya vijijini kutegemea kodi ya mgodi siyo chanzo cha madiwani kukataa tozo hizo kwani muda wowote mgodi huo utaacha uzalishaji na mapato yatazidi kushuka kwahiyo lazima tutekeleze sheria zinazotungwa na bunge” alisema Dc.

Pia mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa viongozi wa serikali pampja na wanasiasa hawana budi kubadilika na kuondokana na kudhalauliana katika utendaji kazi kwa lengo la kuwaletea wanachi maendeleo.
     
Powered by Blogger.