NAIBU KATIBU WIZARA YA ELIMU TEKNOLOJIANA UFUNDI AZINDUA MATUMIZI YA TEHAMA MASHULENI.
NAIBU KATIBU WIZARA YA ELIMU
TEKNOLOJIANA UFUNDI AZINDUA MATUMIZI YA TEHAMA MASHULENI.
Naibu katibu
mkuu Wizara ya elimu sayansi na Teknolojia na ufundi Profesa Simon Msanjila
amesema kuwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari hapa Nchini katika
maeneo ya vijijini watanufaika kwa
kupata elimu ya Kupitia Tehama na Teknolojia ya habari suala ambalo litawezesha
wanafunzi hao kuendana na wakati wa sasa wakiwemo ikiwa ni pamoja na kupata
fursa ya kujifunza masomo ambayo hawajafundishwa kupitia Mtandaohuku wananchi wanazunguka mgodi wa uchimbaji wa
dhahabu ACACIA North Mara uliopo Nyamongo wilayani Tarime Mkoani Mara
wakinufaika na mradi huo kwani nao wataweza kupata fursa ya kujifunza.
Naibu katibu
huyo alisema hayo hayo katika uzinduzi wa Matumizi ya Teknolojia ya habari na
mawasiliano katika Elimu ya Msingi na Sekondari ususani kusoma, kuandika na
Kuhesabu yaani( KKK) ni katika shule ya Msingi Nyamwaga Wilayani Tarime Mkoani
Mara baada ya mfuko wa Dhamana North Mara kutoa Msaada wa Komputa 400 katika
shule 8 katika vijiji vinavyozunguka mgodi wa uchimbaji wa dhahabu Nyamongo
ACACIA Nne zikiwa shule za Msingi na Nne za sekondari pamoja na koputa
mpakato40 kwa walimu wa shule hizo.
Aidha
Msanjila alisema kuwa baada ya huduma hiyo kufika maeneo ya vijijini itaweza
kusaidia wanafunzi hao kusoma masomo hao kwa njia ya mtandao ambayo watakuwa
hawajafundishwa ikiwa ni pamoja na kuendana na Mfumo ulipo kwa sasa wa
Teknolojia.
“Kwa sasa
kila kitu ni mtandao na wanafunzi wa shule za msingi na sekondari vijijini sasa
watanufaika kwa kiasi kikubwa pia mmesema na wanachi watarusiwa kijifunza hivyo
ni jukumu la jamii inayozunguka mgodi kutunza mali hizi ili kizazi kijacho
kiweze kunufaika alisema Msanjila.
John Weigama
ni meneja wa Mfuko wa Dhamana ambao umeweza kufadhili vifaa hivyo vya Tehama
yakiwemo Mabweni kwa lengo la kuboresha
Elimu kwa Mtoto wa kike amesema kuwa mfuko huo unatokana na kampuni mabazo
zimewekeza katika mgodi wa uchimbaji wa dhahabu ACACIA Ukiwemo Mgodi huo
kuchangia mfuko huo asilimia 50 kwa lengo la kusaidia vijiji vyote
vinavyouzunguka mgodi huo ambapoamesema wametoa kipaumbele katika kuboresha
sekta ya Elimu.
Kwa Upande
wake Mratibu wa Mradi huo Piter Bhusene
aliongeza kuwalengo la Mfuko wa Dhamana ambao unatoa huduma kwa vijiji vyote
vinavyozunguka Mgodi wa ACACIA ni kuhakikisha unatekeleza hudum zote za kijamii
ambapo wao wamejikita sana katika kuboresha sekta ya Elimu ambap amesema
kutokana na mfuko huo wameweza kusomesha wanafunzi 68 katika elimu ya juu na 12
Elimu ya Sekondari kutoka katika familia duni kutoka katika vijiji
vinavyozunguka mgodi huo.
Hata hivyp
lengo la Mfuko huo ni kuhakikisha jamii ya Wilaya ya Tarime na Taifa kwa ujumla
wananufaika na Mfuko huo wa huduma ya Jamii ambapo Hamis Lissu ambaye Afisa Elimu Mkoa wa Mara
ameomba mfuko huo kufikia maeneo yote ili uweze kuhudumia wilaya zote za mkoa
wa Mara kwa lengo la kuboresha sekta ya Elimu Msingi na Sekondari.
………….Mwisho…..