MBUNGE HECHE TUNAITAJI MAMBO MANNE YAWANUFAISHE WANACHI WA MARA.
PICHAYAMBUNGE WA JIMBO LA TARIME VIJIJINI JOHN HECHE AKIONGEA HII LEO KATIKA MKUTANO WA HADHARA MJINI SIRARI WILAYANI TARIME MKOANI MARA. |
MBUNGE HECHE TUNAITAJI MAMBO MANNE
YAWANUFAISHE WANACHI WA MARA.
Mbunge wa jimbo la Tarime vijijini John Heche amesema kuwa kwa kushirikiana na wabunge wote wa mkoa wa Mara bila kujali itikadi za vyama vya siasa watahakikisha kwa kipindi cha miaka mitano wanafanyia kazi mambo Manne ili kuweza kuwaletea wanachi maendeleo ya haraka ikiwemo kupatikana kwa Huduma ya Maji yanayotokana na ziwa Victoria katika majimbo yote ya mkoa wa Mara , kuhakikisha Mbuga ya wanyama Serengeti inanufaisha wanachi wote wa Mkoa wa Mara,kukamilika kwa Hospili ya Mkoa pamoja na kujengwa uwanja wa ndege wa kimataifa Musoma.
Hayp
yamebainishwa na mbunge wa jimbo la Tarime Vijiji kupitia CHADEMA Johh
Heche kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika mji wa
sirari kipindi akongea na wanachi wake kuhusu mambo muhimu ambayo wamewekea
mkakati kama wabunge wa mkoa wa Mara watakayohakikisha wanawafanyia wanachi kwa
lengo la kuwaletea maendeleo.
Heche
alisema kuwa mkoa wa Mara umejaliwa kuwa na rasilimali nyingi ikiwemo Dhahabu
kwa upande wa Nyamongo, Mbunge kwa upande wa Serengeti, Maji yanayotokana na
ziwa Victoria hivyo rasilimali hizo hazinabudi kuwanufaisha wananchi wote wa
mkoa wa mara kwa kuhakikisha Huduma za Afya zinzpatikana Huduma za Maji na
kupitika kwa Barabara.
“Bila kujali
itikadi za vyama vyetu wabunge wote tunaotoka mkoa wa Mara tutashirikiana
kupigania mambo hayo manne suala la Maji yanayotokana na ziwa Victoria, Mbuga
ya Serengeti, Uwanja wa Ndege wa kimataifa Musoma pamoja na Hospitali ya Mkoa
ili wananchi waondokane nakufuata Huduma Nairobi na Bugando” alisema Heche.
Kwa upande
wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime Moses Yomami ambaye pia ni
dawani wa kata ya Nyamwaga alisema kuwa atahakikisha anawachukulia hatua kali
kwa baadhi ya watendaji wa serikali ambao wamekuwa wabadhilifu kwa kuujumu fedha za serikali pamoja na wanachi jambo
ambalo linakwamisha maendeleo.
Mases
alisema kuwa katika kuzungukia miradi ya wanachi wameweza kugundua changamoto
mbalimbali ukiwemo ubadhilifu wa fedha za wanchi na serikali hivyo amehaidi
kuwa kupitia vikao vya madaiwani watahakikisha wanawashughulikia baadhi ya
watendaji ambao wamekiuka taratibu za utumishi.
“Hatuwezi
kuvumilia kila siku baadhi ya watendaji ambao wanaiba fedha za serikali na
kusababishia Halmashauri hasara kubwa lazima tuwawajibishe kwa ajili ya kulinda
heshima ya Halmashauri” alisema Moses.