JESHI LA POLISI LAMTUNUKU TUZO MAMA ALIYEPAMBANA NA JAMBAZI.
PICHA YA KAMANDA WA POLISI MKOA WA KIPOLISI TARIME RORYA GEMINI MUSHY AKIKABIDHI ZAWADI YA SHILINGI LAKI TANO KWA MAMA SHUJAASOPHIA STEVEN ALIYEPAMBANA NA JAMBAZI NA KUFANIKIWA KUMUNYANG'ANYA BUNDUKI NA RISASI 27.
JESHI la
Polisi mkoa wa Kipolisi Tarime/Rorya limemtunuku hati ya tuzo ya ujasili na
fedha laki tano mwanamke Sophia Stephen(46)
mkazi wa kijiji cha Buriba Wilayani Tarime aliyemyang’anya bunduki
jambazi wakati jambazi akijaribu kupambana na mama huyo baada ya kumvamia
Nyumbani kwake.
Kamanda wa
Polisi mkoa wa Kipolisi Tarime/Rorya Geminis Mushy amesema kuwa kutokana na
ujasili wake bila kuogopa kuwa ni mwanamke alipambana na majambazi na
kufanikiwa kuchukuwa bunduki aina ya SMG/SR na Risasi 27 jambo ambalo limevuta
hisia kwa watu wengi.
Mushy amesema kuwa mnamo April 9,2016 majira ya saa mbili usiku mama huyo akiwa kwenye shughuli zake za biashara kwenye duka
lake nyumbani kwake alivamiwa na Gisanja Matinde(19) mkazi wa Getenga akiwa na
wenzake 2 na kumyang’anya pesa 80,000.
“Walimwelekezea
silaha hiyo wakimtishia asipowapa pesa watamuua,walivamia pia duka la Zaituni
Magasi(29) na kumyang’anya 100,000
hata hivyo walipiga yowe wananchi wakafika kusaidia na askari wa dolia na Jambazi Gisanja
akakamatwa bunduki ni SMG namba UK 115 ikiwa na risadi 27”alisema.
Hata hivyo
mwanamke huyo alisema kuwa ameshajitoa muhanga na nijasiri kwa madai kuwa tukio
la kuvamiwa ni la mara ya pili kwake ila
akawaomba wananchi mtu anapopiga yowe ya kuvamiwa wajitokeze kusaidia kwakile
alichoeleza wananchi wangechelewa eneo la tukio huwenda angeuwawa.
Kamanda
Mushy alimpongeza mwanamke huyo kwa ujasiri wa ajabu wa kukabiliana na jambazi huyo
na hatimaye kuokoa silaha na risasi nakwamba jeshi la polisi linatambua
mafanikio hayo.