WAZIRI JENISTA, SERIKALI ITAHAKIKISHA WANANCHI WAKE HAWAFI NA NJAA.
PICHA YA WAZIRI WA NCHI OFISI YA WAZIRI MKUU SERA, URATIBU NA BUNGE KAZI, AJIRA NA WALEMAVU JENISTA MHAGAMA AKIONGEA NA WATUMISHI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA ITILIMA MKOANI SIMIYU HII LEO KATIKA ZIARA YAKE
Kupitia
waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri mkuu Sera uratibu na
Bunge,Kazi ajira vijana na walemavu, serikali imesema kuwa haitaruhusu mtanzania
yeyote kufariki kwa janga la janga bali serikali itaendelea kutoa msaada wa chakula pale mahafa
yanapotokea kwa wakati kwa lengo la kuwanusuru wahanga.
Hayo
yamebainishwa na waziri wa Ofisi ya Waziri mkuu
Sera , Bunge,Kazi ajira vijana na walemavu Jenista Mhagama alipokuwa
kwenye ziara mkoani Simiyu.
Waziri huyo
alisema kuwa mpaka sasa serikali inachakula cha kutosho hivyo itahakikisha
wananchi wake pale wanapokumbwa na janga la njaa wanapata chakula mara moja kwa
lengo la kunusuru maisha yao.
Aidha waziri huyo katika juhudi za kukomboa
mwananchi ili aweze kuondokana na janga la njaa amezitaka Halmashauri zote mkoa
wa simiyu kupitia wataalamu wake
kuanzisha mara moja kuanzisha kilimo cha kisasa na chenye tija huku wakitoa kipaumbele kwa mazao yanayokomaa
kwa muda mfupi.
“Hapa
nimezunguka tayari nimeona mabonde mazuri ya kulima mazao mengi yakiwemo ya
kukomaa kwa muda mfupi hivyo nagiagiza Halmashauri zote kupitia wataalamu wa
kilimo kwenda kwa wananchi na kutoa elimu juu ya matumizi bora ya kilimo cha
kisasa na utumiaji wa mbolea katika upandaji wa mazao hayo kwa lengo la
kuongeza tija katika uzalishaji wa chakula hicho” alisema Wziri.
Hata hivyo
mhagama ameweza kuziagiza Halmasauri hizo kufufua kamati za mahafa kuanzia ngazi ya
vijiji na kata nakuanza kufanya kazi mara moja ili pale mahafa yanapotokea
taarifa ziweze kufika mapema mahali panapohusika huku hatua za awali
zikiwazimeisha chukuliwa kwa lengo la kunusuru wahanga wa tukio katika eneo huska.
Kwa upande
wake mkurugenzi wa Halmashauri ya Itilima John Aloyce
kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Itilima Ponsiano Nyami akisoma taarifa mbele ya waziri wa wa Ofisi
ya Waziri mkuu Sera , Bunge,Kazi ajira
vijana na walemavu anasema kuwa kuvamiwa kwa mashamba ya mazao ya chakula na wanyama aina ya Tembo katika vijiji
vinavyopakana vimepakana na hifadhi kunaweza
kuwa chanzo cha kusababisha njaa.
Ziara hiyo
ya waziri imeweza kuwashirikisha wabunge wawilia akiwemo mbunge wa viti maalumu
CHADEMA Mkoa wa Simiyu Gimbi Masaba pamoja na Mbunge wa jimbo la Itilima Njaro
Daud ambapo wabunge ao wamezidi kuwaomba
watendaji kusimamia ipasavyo msaada wa chakula
cha aina yeyote pale kinapotoka serikalini ili kiweze kuwafikia wananchi
huku wakiomba kuongezwa kwa wataalamu wa kilimo katika sekta ya kilimo na
mifugo kwa lengo la kufanya kzi kwa ufanisi.