WATUMISHI WA MAHAKAMA WATAKIWA KUTENDA HAKI KWA WANANCHI.

PICHA YA HAKIMU MKAZI  MAHAKAMA YA MWANZO TARIME MJINI DENIS DIBOGO WENJE KUSHOTO AKIWA AMESHIKILIA BANGO LENYE UJUMBE NI KATIKA VIWANJA VYA MAHAKAMA YA WILAYA KABLA YA MAANDAMANO KUELEKEA VIWANJA VYA SERENGETI MJINI TARIME KWA LENGO LA UZINDUZI WA WIKI YA SHERIA NCHINI,



WATUMISHI WA MAHAKAMA WATAKIWA KUTENDA HAKI KWA WANANCHI.







Watumishi wa mahakama wametakiwa kufuata kanuni Taratibu na sheria zinazotungwa na bunge kwa mjibu wa sheria ili kuweza  kuweza kuwasaidia wanachi katika mashauri yanayotolewa katika mahakama mbalimbali ikiwa ni pamoja na wananchi  kufuata sheria kwa lengo la kuishi kwa Upendo na Amani .




Kauli hiyo imetolewa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Tarime John Marwa kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Tarime Glorius Luoga katika uzinduzi wa wiki ya Sheria ambapo Wilayani Tarime  uzinduzi huo kiwilaya umefanyika kwenye  viwanja vya Serengeti Mjini Tarime baada ya maandamano kutoka viwanja vya Mahakama ya Wilaya.







Aidha Katibu Tawala alisema kuwa Pamoja na mahakama kupewa ridhaa ya kutoa haki kumekuwepo na changamoto kwa baadhi ya watumishi wa mahakama wamekuwa wakikiuka sheria na taratibu za utumishi wa Umma hivyo ametumia fursa hiyo kuwahasa watumishi hao kutenda haki kulingana na mujibu wa sheria.




Hata hivyo Marwa kwa niaba ya mkuu wa Wilaya ya Tarime aliongeza kuwa  kila mwananchi ana wajibu wa kufuata sheria na taratibu za Nchi kwa lengo la kuishi kwa Amani.




“Katika hili kama kun badhi ya watumishi wanaokiuka sheria ahawana budi kujirekebisha kwani serikali kwa kushirikiana na Rais wa Nchi hawatafumbiwa macho” alisema Marwa.







 Kwa upande wake  Hakimu mkazi mfawidhi Wilayani Tarime Martha Mpaze amewataka wananchi kuwa waone mahakama ni chombo huru ni kipo kwa ajili ya kutoa haki na kuwataka wanachi kutumia mahakama yao kwa ajili ya kupata haki.




Aidha Martha alisema kuwa katika maadhimisho hayo ambayo yatachulua takribani wiki moja ambapo kilele chake ni Feburuari Nne Mwaka huu amewataka wananchi wenye mashauri mbalimbali ikiwemo migogoro ambayo inatakiwa kutatuliwa na mahakama kufika katika viwanja vya Serengeti pamoja na viwanja vya mahakama Wilayani Tarime.




Hata hivyo Hakimu huyo alisema kuwa watafikia vyuo mbalimbali, Magereza pamoja na Shule za Msingi na sekondari kwa lengo la kutoa Elimu kuhusu mahakama.




Naye Hakimu Mkazi Mahakama ya Mwanzo Tarime Mjini Denis Dibogo Wenje anaeleza lengo la maadhimisho hayo kuwa ni kuhakikisha kila mwananchi anatambua umhimu wa mahakama pamoja na taratibu zinazotakiwa kufuatwa kwa lengo la kupata huduma stahiki.




“Tutaweza kutoa Elimu katika Wilaya ya Tarime pamoja na Rorya kwani mahakama yetu inafanya kazi katika Wilaya Mbili na lengo ni kuhakikisha wananchi wanatumia mahakama yao ili kuweza kupata haki kulingana na ujumbe ambao tumebeba kwa leo kupitia mabango yetu” alisema Wenje.







Bony Matto ni mkurugenzi wa kituo cha binadamu (SHEHABITA) alisema kuwa wananchi wamekuwa na mwitikio mdogo kwa dhana kuwa mahakama ni sehemu ya kuogopwa wakati fursa kama hiyo wangweza kuitumia kwa lengo la kupata mashauri ili kuweza kupata mwanga na kuweza kuweza kufuatilia kesi zao ili ziweze kutolewa mashauri.




Nyamwise Marwa ni moja kti ya wanachi ambapo alisema kuwa amefurahi kitendo cha mahakama kuandaa maadhimisho hayo katika viwanja vya wazi na kuwataka wananchi kutoa maoni yao jambo ambalo halijawahi kufanyika.



Mimi tangu kuzaliwa sijawahi kuona mahakama inafanya kitendo hiki cha leo hivyo hii hatua itafanya wananchi kuwa na imani na mahakama zao alisema Nyamwise.







Katika maadhimisho ya wiki ya sheria Nchini kauli mbiu ni  Huduma za haki kumlenga mwananchi wajibu wa mahakama na wadau ambapo kilelele chake ni Feburuari  Nne Mwaka huu.

Powered by Blogger.