WAFANYABIASHARA WA MIFUGO WATOA KILIO KWA MAGUFULI.

PICHA YA MBUNGE WA VITI MAALU MU MKOA WA SIMIYU GIMBI MASABA AKIONGEA NA WANANCHI KATIKA ZIARAYA KUKAGUA MNADA WA NG'OMBE HALMASHAURI YA MJI WA BARIADI MKOANI SIMIYU.



WAFANYABIASHARA WA MIFUGO WATOA KILIO KWA MAGUFULI.

Wafanya bihashara wa mifugo na wafugaji katika mji wa Bariadi mkoani Simiyu wameiomba Serikali ya Magufuli kusikilza kilio chao kuhusu kutozwa ushuru mkubwa kulingana na mauzo yao katika mnada wa Bariadi mkoni  humo huku wakiomba kuwepo  tofauti makato ya ushuru kati ya Muuzaji na Mununuzi pamoja na mifugo inayokosa wateja na kurejeshwa nyumbani  kwa kutolipia awamu ya pili  ushuru.

Hayo yamebaimishwa na wafanyabihasahara hao pamoja na wafugaji katika soko la Bariadi ambalo ni maarufu kwa mnada wa uzaji wa Ngombe, Mbuzi pamoaja na Kondoo,  kipindi wakiongea na mbunge wa Mkoa wa Simiyu kupitia CHADEMA Gimba Massaba alipotembelea soko hilo ili kuweza kubaini changamoto zinzowakumba wafanya biashara hao wamesema kuwa kutozwa kwa ushuru mkubwa imekuwa kero hivyo wamemwomba rais Magufuli kusikiliza kilio chao kwa lengo la kupunguziwa ushuru.

Aidha wafanyabiashara hao wamesema kuwa katika mnada huo kila  Ng’ombe mmoja utozwa shilingi 6000, Mbuzi na Kondoo 2000 wakati wa kuingiza mifugo na kutoa mifugo katika mnada huo aidha uuze au usiuze mifugo hao suala ambalo ni changamoto kubwa kwa wafanyabihashara hao.

Hata hivyo baadhi ya Wafugaji wamedai kuwa baadhi yao siyo wafanyabihashara kulingana uchumi kushuka na janga la njaa uamua kutoa mifugo yao kwenye zizi ili kupeleka mnani hapo kwa ajili ya kupata kipato lakini kinachowashangaza hata mifugo hiyo ikikosa wateja lazima walipe ushuru kwa kila Ngombe Mmoja shilingi 6000.

“Mnada huu umekuwa kero kubwa kwetu sisi wafugaji na wafanyabiashara kitendo cha kuingiza mifugo unalipa 6000 kwa kila Ngombe Mbuzi na kondoo 2000kila mmoja na badae kama wateja wamekosa lazima ulipe awamu ya pili sasa hii ni nchi gani na wakati rais anatetea wanyonge sisi hatukatai kulipa ushuru lakini kuwepo utaratibu mzuri usiokandamiza wananchi tumechoka kweli” walisema Wananchi hao.

Amani Sopu ni mwenyekiti wa wachinjaji Katika mji wa Bariadi ameongeza kuwa wamekuwa wakilipia ushuru kila mahari  kukiwemo katika Machinjio, Buchani Pamoja na Eneo la Mnada suala ambalo limekuwa kero kwao na kuiomba serikali kuingilia kati kwa lengo la kutatua changamoto hiyo.

“Mimi ni mwenyekiti wa wachinjaji lakini kero tumelalamika mda mrefu na tunalipa ushuru wakati wa kununua Mifugo tukienda machinjio tunalipa tena, tukileta nyama buchani tunalipa tena bado tumelipia leseni za bias” alisema Amani.

Kwa upande wake mbunge wa viti maalumu mkoa wa Simiyu Gimbi Masaba kiwa katika ziara ya kutembelea soko hilo ili kubaini changamoto zinzowakabili alisema kuwa serikali haijajenga mazingira rafiki kwa lengo la kuendeleza mnada huo suala ambalo linapaswa asilimia kadhaa zinzzotokana na makusanyo hayo ziweze kulidi mahari hapo kwa lengo la kuboresha manada uo lakini  jambo hilo halifanyiki bali kila kunakokucha wanapandisha ushuru wa kila aina wakiwemo wafanya bihashra wadogo wadogo.

“Kwa sasa mwananchi anatozwa ushuru mkubwa hivi na wengi hapa ni wafugaji kulingana na ugumu wa maisha kwa sasa wameamua kutoa mifugo kwenye zizi ili wakauze na kuwez kuendesha familia zao na hapa tumeona auze hasiuze lazima ushuru akalipie je hawa wafugaji fedha wanatoa wapi kama mifugo yao haijauzwa huu ni wizi” alisema Mbunge.

Gumada Daudi ni mzabuni wa mnada huo amesema kuwa mnada huyo amesema kuwa changamoto za ukosefu wa uzio unampa shida katika kukusanya ushuru kwani hawezi kutofautisha kati ya Muuzaji na Mnunuzi.
“Halmashauri ingeweza kuboresha mazingira ya Mnada kukawepo mazingira rafiki nadhani ingeweza kusaidia kwa kiasi kikubwa na tungeweza kutengeneza utofauti kati ya Mmunuzi la muuzaji pamoja na Mifugo inayokosa wateja na jambo ili linapelekea niweze kuajili wafanya kazi wengi na baadhi ya wafanyabihashara hawalipi hivyo mimi kama mzabuni naingia hasara kubwa” alisema Daud.

Sanjari na hayo mzabini huyo aliongeza kuwa yeye mapata nayokata ya Halmashauri ya mji wa Bariadi ni silingi 5000 ampapo 1000 uchukuliwa na watu wa idara ya mifugo suala ambalo upelekea kufikia kiasi cha shilingi 6000.


Powered by Blogger.