MBUNGE CHADEMA SIMIYU ATOA MSAADA WA VITI VYENYE THMANI YA SHILINGI ZAIDI YA MILLIONI MBILI.
PICHA YA MBUNGE WA VITI MAALUMU MKOA WA SIMIYU GIMBI MASABA AKIKABIDHI MSAADA WA VITI 150 KWA UONGOZI WA CHAMA WILAYA YA ITILIMA KATIKATI NI KATIBU WA CHADEMA WILAYA YA ITILIMA MIGASA MIPAWA ANAYEFUATIWA NI KATIBU MWENEZI WILAYA MASUKE GUBI.
MBUNGE CHADEMA SIMIYU ATOA MSAADA WA VITI VYENYE THMANI YA
SHILINGI ZAIDI YA MILLIONI MBILI.
Katika kuboresha
miundombinu ya chama mbunge wa viti maalumu CHADEMA mkoa wa Simiyu Gimbi Masaba
ametoa msaada wa viti 150 vya plastiki vyenye thamani ya shilingi 2,475,000
katika ofisi ya kata ya Luguru.
Akikabidhi viti
hivyo kwa wananchama hao wilaya ya Itilima
mbunge huyo alisema kuwa ameamua
kutoa msaada huo kwa lengo la kuimalisha chama kwani kata hiyo ilikuwa
ikikumbwa na vifaa vya chama vikiwemo viti vya kukalia pale panapokuwepo
mikutano.
“Nimeweza kutoa
viti hivi lakini vitaendelea kusaidia wanachama wa chama cha CHADEMA pia
vitaweza kutatua changamoto kubwa popote pale panapofanyika mkutano wa chama”
alisema Mbunge huyo.
Kabla ya
kukabidhiwa msaada huo kiliendelea kikao cha ndani kwa ajili ya kuzungumzia
mstakabali wa chama hico baada ya uchaguzi wa mwaka jana ambapo kikao hicho
kimeweza kupatanisha viongozi mbalimbali ambao walikuwa na mpasuko mkubwa kutokana
na makundi yaliyokuwepo kipindi cha uchaguzi.
Aidha wananchama
hao wameaswa kuendela kusoma mara kwa mara katiba ya chama hicho kwa lengo la
kufuata maadili ya chama ikiwa ni pamoja na kuondokana na makundi yasiyokuwa ya
misingi kwani wakati wa siasa umeisha bali kwa sasa waweze kufanya kazi kwa
ajili ya maendeleo ya wananchi wao.
Kikao hicho
kimeweza kushirikisha madiwani walishinda uchaguzi wa mwaka jana na
walioshindwa wenyeviti wa vijiji, makatibu kata na wenezi kata kwa lengo la
kufanya tathimini na kubaini changamoto zilizowafanya kushindwa.
Hata hivyo
katika kikao hicho mbunge wa viti maalumu chadema mkoa wa simiyu Gimbi Masaba
alisema kuwa atahakikisha anatumia mshahara wake kwa lengo la kujenga chama
ambapo alisema kuwa kwa kuwa chadema walilenga kuwa wkishinda urais wenyeviti
wa vijiji wangeweza kulipwa mshara hivyo amesema kuwa wenyevitikutoka wilaya ya
Itilima mkoani humo takribani 52 atahakikisha kila mwezi anawalipa shilingi 20,000
huku akitoa ahadi ya pikipiki moja kwa mwenezi wa chama wilaya ya Itilima
Masuke Gubi .
“Mimi sina mfuko
wa jimbo lakini niatendelea kutumia mshahara wangu kwa lengo la kujenga chama”
alisema Gimbi.