MATIKO AKABIDHI MIFUKO 20 YA SARUJI KUNUSURU SHULE YA MSINGI.
PICHA YA MBUNGE WA JIMBO LA TARIME MJINI ESTHER MATIKO AKIKABIDHI MIFUKO 20 YA SARUJI KATIKA SHULE YA MSINGI MASURULA KATA YA NYANDOTO HALMASHAURI YA MJI WA TARIME BAADA YA MADARASA MAWILI KUBOMOLEWA NA MVUA ZINZOENDELEA KUNYESHA.
MATIKO AKABIDHI MIFUKO 20 YA SARUJI
KUNUSURU SHULE YA MSINGI.
Mbunge wa
jimbo la Tarime mjini Esther Matiko amekabidi mifuko 20 ya saruji yenye thamani
ya shilingi laki nne kwa lengo la kunusuru shule ya msingi Masurula kata ya
Nyandoto katika Halmashauri ya mji wa Tarime akiwa na lengo kwamba januari
wanafunzi hao wapate fursa ya kuendelea na masomo.
Kulingana na
Mvua kubwa zilizokuwa zikinyesha maeneo mbalimbali ziliweza kubomoa madarasa
mawili katika shule ya msingi masurula hivyo kunusuru hali hiyo mbunge wa jimbo
la Tarime mjini Esther Matiko ametoa msaada wa mifuko 20 ya saruji yenye thmani
ya shilingi 400,000 ili shule .
itakapofunguliwa rasmi wanafunzi waendeleena masoma kama kawaida.
“Mimi ni
mbunge wa wananchi wote bila kujali
itaikadi za vyama nitaendelea kushirikiana na kila mwananchi wangu katika jimbo
langu ili kuhakikisha tunatatua changamoto zinazowakabili wananchi wangu”
alisema Matiko.
Aidha mbunge
huyo aliongeza kuwa jukumu la kiongozi ni kuwatumikia wananchi kwa kutatua
changamoto zinazowakumba katika sekta za Elimu, Maji na Afya.
Kwa upande
wake mwenyekiti wa mtaa wa masurula kata ya Nyandoto (CCM) Marwa jackson baada ya kupokea msaada huo wa
mifuko 20 ya saruji lisema kuwa juhudi ambazo amezianza mbunge uyo zinzidi
kuwapa matumaini wananchi wake bila ya kujali kuwa mitaa hiyo inaongozwa na
chama cha mapinduzi angali mbunge ni wa chama cha upinzani.
“Tunazidi
kutoa shukrani zetu nyingi kwa mbunge
wetu kwa kutambua changamoto hii na kuweza kutoa msaada wa saruji mifuko 20
itaweza kusaidia na kwa sasa mafundi wataendelea na ujenzi wa madarasa mawili
kwani shule hii inamapungufu katika madarasa” alisema Mwenyekiti.
Kwa upande
wake diwani wa viti maalumu kupitia (CHADEMA) Tekra Joanes katika kuunga juhudi
za mbunge wa jimbo la Tarime mjini alitoa gari moja la mchanga ili kuweza kufanikisha
ujenzi huo.
Hawa watoto
ni wetu na sisi kama viongozi ambao tumepewa ridhaa ya kuongoza hivyo ni
wajjibu wetu kuendelea kuunga mkono katika suala zima la maendeleo ikiwa ni
pamoja na kutoa msaada wa vifaa katika maeneo ambao yanakumbwa na mahafa
makubwa” alisema Tekra.
Nao baadhi
ya wazazi wa watoto wanaosoma shulenkulingana na serikali kupunguza michango
mashuleni watahikikisha watoto wao wanapata Elimu kwa lengo la kuwakombo na
kwaandalia maisha yao ya badae.
….Mwisho…..