SOMANDA YAKABILIWA NA UPUNGUFU WA DAWA NA VIFAA TIBA.
PICHA YA MBUNGE WA VITI MAALUMU MKOA WA SIMIYU GIMBI MASSABA AKIONGEA NA MMOJA KATI YA MAMA AMBAYE ANAMUUGUZA MTOTO WAKE JANA ALIPOTEMBELEA HOSPITALI YA SOMANDA MJINI BARIAD. |
SOMANDA
YAKABILIWA NA UPUNGUFU WA DAWA NA VIFAA TIBA.
Katika
kuboresha sekta ya Afya pamoja na utendaji kazi wake serikali imeombwa kutoa
dawa kwa wakati ili kuondoa changamoto ya upungufu wa madawa pamoja na vifaa
tiba vikiwemo vifaa vya kupimia damu ili kubaini maambukizi ya magonjwa aina
mbalimbali, vikiwemo virusi vya Ukimwi
katika Hospitali ya Somanda Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.
Hayo
yamebiainika katika ziara ya Mbunge wa viti maalumu CHADEMA Mkoa wa Simiyu
Gimbi Massaba alipokuwa anatembelea Hospitalini hapo kwa lengo la kubaini
changamoto zinazoikabili Hospitali hiyo
kwa lengo la kuzizungumzia changamoto hizo pale bunge la jamhuri ya
muungano wa Tanzania litakapoaanza rasmi.
Katika zira
hiyo ambao inaendelea Mkoani hapa mbunge huyo ameweza kutmbelea hodi ya Watoto,
pamoja na wazazi huku akitoa msaada wa mafuta ya kujipaka, Dawa ya Meno,
Miswaki,sabuni za kufua pamoja na Maji ya kunywa huku akitumia fursa hiyo kuomba serikali kkuliona jambo ili kupunguza
changamoto na kulalamika kwa wananchi ho.
“Hiki kilio
cha upungufu wa madawa sasas kimekuwa kilio cha kila siku hivyo serikali ya
magufuli haina budi kujipanga kikamilifu ikiwa ni pamoja na kuleta dawa kwa
wakati na dawa za aina zote ili kuwapunguzia ghala ambazo siyo za lazima
wanachi wangu” alisema Mbunge.
Hata hivyo
mbunge huyo katika kuzunguka kwenye hodi ya wazazi amekutana na mama mmoja
anayejulikalikana kwa jiana la stella john mkazi wa Bariadi mjini ambaye amepigiwa vikali na mmewe huku akiwa
na ujauzito wa miezi tisa suala ambalo linaweza kusababisha mama huyo
kutojifungua salama na kulilaani vikali huku akiomba serikali kukemea vitendo
vya ukatili wa kijinsia pamoja na mfumo dume na elimu zikitolewa maeneo ya
vijijinini.
Serikali kwa
kushirikiana na mashirika mbalimbali hawana budi kutilia mkzo suala la kupinga
mfumo dume ambao umejikita hapa kwa mkoa wa simiyu bado Elimu hiko chini hivyo
Elimu ikitolewa vyema ukatili wa kijinsia utapungua kama maeneo mengine.
Saidi
Mlowosha ni kaimu mganga mkuu akitaja changamoto zinzowakabili alisema serikali
haina budi kutatua suala zima za upungufu wa madawa pamoja na vifaa tiba ili
kuondoa lawama kwa wananchi.
“Sisi
tunafuata sheria za manunuzi na kanda ya ziwa tunachulia mwanza Msd lakini
unakuta baadhi ya dawa hazipo na hatuna ruhusa ya kununua dawa nje hata Msd
mwanza mpaka wapate kibali kutoka makao makuu na inachukua mda hivyo serikali
iliangalie suala hilo ili kuokoa maisha ya watanzania wote make kilio hiki ni
Nchi nzima” alisema Kaimu Mganga mkuu.
Nao baadhi
ya wananchi waliopokea msaada huo wamezidi kutoa shukrani kwa mbunge huyo huku
wakipongeza wataalamu kuwa wanatoa huduma kwa wakati japokuwa changamoto ya
ukosefu wa baadhi ya dawa ndo kubwa suala ambalo linapelekea kwenda kununua
dawa maduka ya binafsi
“Tatizo
kubwa hapa ni upungufu wa madawa suala ambalo linapelekea kupimwa na kuelekezwa
kwenda kununua madawa katika maduka ya watu binafsi serikali ya magufu sikiliza
kilio cha wananchi” walisema wananchi ho.
…….Mwisho……