Na Frankius Cleophace SIMIYU. GIMBI MAGUFULI ONGEZENI MISHAHARA KWA WALIMU WA VISIWANI NA MAENEO YA PEMBEZONI. Kulingana na kauli ya Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania john Magufuli ya hapa kazi Mbunge wa viti maaulumu kupitia chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA mkoa wa Simiyu Gimbi Dotto amesema kuwa rais hana budi kuangalia upya mishahara pamoja na posho za walimu waliko maeneo ya visiwani na maeneo ya vijiji vya pembezoni kwa lengo la kuboresha utendaji kazi kulingana na kauli mbiu yake huku sekta za afya pamoja na miundo mbinu ya maji na barabara ikiboreshwa zaidi maeneo ya vijijini. Hayo yamebainishwa kipindi mbunge akiongea na waandishi wa habari mkoani simiyu kuhusu ziara yake ya kibunge ambayo inatarajia kuanza hii leo kwa lengo la kubaini kero za wananchi ili kuweza kuzisemea bungeni pale bunge la jamhuri ya muungano litakapoanza ras. Mbunge huyo wa viti maalumu alisema kuwa kwa sasa nafanya kazi za wananchi wote bila kujali itikadi za vyama kwa lengo la kuwaletea wananchi maendeleo lakini ameongeza kuwa kulingana na kasi ya rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania hana budi kuangali upya mishahara ya walimu walioko visiwani na maeneo ya pembezoni kwani wanafanya kazi katika maeneo magumu ikiwa ni pamoja na kulipa madai ya walimu wote hapa Nchini ili kuboresha sekta ya Elimu kulingana na kauli mbiu ya Elimu bure. Mbunge huyo alissema kuwa kuwa katika ziara yake ataweza kutembelea Sekta ya Afya, Elimu, kuangalia miundombinu ya barabara pamoja na kutembelea magereza huku akisikiliza kero za wananchi ikiwa migogoro ya Ardhi kuharibiwa kwa mazao ya wananchi na wanayamapori Hata hivyo mbunge huyo alimtaka Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi na mwenzake kutatua migogoro ya ardhi huku wakiweka mikakati ya pamoja ikiwa ni pamoja na kuangalia baadhi ya matajili ambao wamepokonya ardhi ya wananchi. “Kuna baadhi ya ardhi ya wananchi imepokonywa na matajiri wachache waziri mwenye dhamana hana budi kuingilia kati ili wananchi wapewa haki yao” alisema Ngimbi. Hata hivyo mbunge huyo amemwomba rais pia kuendelea mchakato wa katiba mpya kulingana na maoni ya wananchi yaliyomo kwenye rasmi ya Warioba. “Tunamtaka Rais Magufuli kuanzisha upya mchakato wa upatikanaji wa Katiba Mpya, kwa kutumia maoni ya wananchi yaliyomo kwenye Tume ya Rasimu ya Jaji Joseph Sinde Warioba,Tunahitaji suala hili litiliwe mkazo na Serikali iliyopo madarakani, ili kuondokana na Katiba ya sasa, ambapo baadhi ya ibara na vifungu vyake vinaonekana kupitwa na wakati, hivyo kukandamiza demokrasia na kuminya haki za raia za Watanzania” alisema. Aliongeza kuwa Katika Katiba hiyo Mpya, Rais apunguziwe madaraka, ushindi wa Rais uhojiwe mahakamani, Tume huru ya Uchaguzi na mambo mengine muhimu yatakayopendekezwa na wananchi kwa maslahi ya taifa. …………MWISHO………

PICHA YA MBUNGE WA VITI MAAKUMU MKOA WA SIMIYU GIMBI DOTTO WA TATU KUSHOTO AKIONGEA NA VYOMBO VYA HABARI JANA MJINI BARIADI.



GIMBI MAGUFULI ONGEZENI MISHAHARA KWA WALIMU WA VISIWANI NA MAENEO YA PEMBEZONI.

Kulingana na kauli ya Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania john Magufuli ya hapa kazi Mbunge wa viti maaulumu kupitia chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA mkoa wa Simiyu  Gimbi Dotto amesema kuwa rais hana budi kuangalia upya mishahara pamoja na posho za walimu waliko maeneo ya visiwani na maeneo ya vijiji vya pembezoni kwa lengo la kuboresha utendaji kazi  kulingana na kauli mbiu yake huku sekta za afya pamoja na miundo mbinu ya maji na barabara ikiboreshwa zaidi maeneo ya vijijini.

Hayo yamebainishwa kipindi mbunge akiongea na waandishi wa habari mkoani simiyu kuhusu ziara yake ya kibunge ambayo inatarajia kuanza hii leo  kwa lengo la kubaini kero za wananchi ili kuweza kuzisemea bungeni pale bunge la jamhuri ya muungano litakapoanza rasmi.

Mbunge huyo wa viti maalumu alisema kuwa kwa sasa nafanya kazi za wananchi wote bila kujali itikadi za vyama kwa lengo la kuwaletea wananchi maendeleo lakini ameongeza kuwa kulingana na kasi ya rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania hana budi kuangali upya mishahara ya walimu walioko visiwani na maeneo ya pembezoni kwani wanafanya kazi katika maeneo magumu ikiwa ni pamoja na kulipa madai ya walimu wote hapa Nchini ili kuboresha sekta ya Elimu kulingana na kauli mbiu ya Elimu bure.

Mbunge huyo alissema kuwa  kuwa katika ziara yake ataweza kutembelea Sekta ya Afya, Elimu, kuangalia miundombinu ya barabara pamoja na kutembelea magereza huku akisikiliza kero za wananchi ikiwa migogoro ya Ardhi kuharibiwa kwa mazao ya wananchi na wanayamapori.

Hata hivyo mbunge huyo alimtaka   Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi na mwenzake kutatua migogoro ya ardhi huku wakiweka mikakati ya pamoja ikiwa ni pamoja na kuangalia baadhi ya matajili ambao wamepokonya ardhi ya wananchi.

 “Kuna baadhi ya ardhi ya wananchi imepokonywa na matajiri wachache waziri mwenye dhamana hana budi kuingilia kati ili wananchi wapewa haki yao” alisema Ngimbi.  

Hata hivyo  mbunge huyo amemwomba rais pia kuendelea mchakato wa katiba mpya kulingana na maoni ya wananchi yaliyomo kwenye rasmi ya Warioba

Tunamtaka Rais Magufuli kuanzisha upya mchakato wa upatikanaji wa Katiba Mpya, kwa kutumia maoni ya wananchi yaliyomo kwenye Tume ya Rasimu ya Jaji Joseph Sinde Warioba,Tunahitaji suala hili litiliwe mkazo na Serikali iliyopo madarakani, ili kuondokana na Katiba ya sasa, ambapo baadhi ya ibara na vifungu vyake vinaonekana kupitwa na wakati, hivyo kukandamiza demokrasia na kuminya haki za raia za Watanzania” alisema.

Aliongeza kuwa Katika Katiba hiyo Mpya,  Rais apunguziwe madaraka, ushindi wa Rais uhojiwe mahakamani, Tume huru ya Uchaguzi na mambo mengine muhimu yatakayopendekezwa na wananchi kwa maslahi ya taifa.


  …………MWISHO………
Powered by Blogger.