MBUNGE WA CHADEMA ASHIRIKI CHAKULA CHA PAMOJA NA WATOTO WALEMAVU.

PICHA YA MBUNGE WA VITI MAALUMU MKOA WA SIMIYU GIMBI MASSABA AKISHIRIKI CHAKULA CHA PAMOJA NA WATOTO WENYE ULEMAVU WA NGOZI WANAOLELEWA KATIKA KITUO CHA BIKIRA MARIA LAMADI MKOANI SIMIYU SIKU YA KRISMAS.
MBUNGE WA CHADEMA ASHIRIKI CHAKULA CHA PAMOJA NA WATOTO WALEMAVU.

Mbunge wa viti maalumu mkoawa simiyu CHADEMA Gimbi Massaba ashiriki chakula cha pamoja na watoto wenye ulemavu wa ngozi (Albinism)kwa lengo la kusherekea sikuku ya krismas ikiwa ni pamoja na kutaoa zawadi mbalimbali kwa lengo la kuwafariji watoto hao wanaishi katika kaituo cha kulelea watoto ch Bikira Maria kilichopo Lamadi.

Akiongea na watoto hao baada ya kushiriki chakula cha pamoja Mbunge huyo wa viti maalumu alisema kuwa ameaamua kufanya hivyo kwa lengo kuwafariji watoto hao ambao wako katika kundi maalumu kwani jamii imekuwa ikiwatenga na kuwabagua kutokana na imani potofu.

“Watoto hawa ni wa kwetu pia sisi kama viongozi wa kijamii hatuna budi kushiriki chakula cha pamoja ikiwa ni pamoja na kutoa misaada mbalimbali ili watoto hawa waweze kukua vyema na baadhi hawana wazazi wao hivyo tukitumia nafasi hii kukaa nao na kula chakula cha pamoja wanafurahi sana” alisema Gimbi.

Kituo hicho cha bikira maria kina jumla ya wototo 54 wakiwemo wenye ulemavu wa Ngozi, utindio wa ubungo na walemavu wa viungo vya mwili, Mratibu wa kituo hicho Belensi China alisema kuwa kituo hicho kinakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya ukosefu wa uzio kwa lengo la kuweka watoto hao salama kwani wanawindwa.

Hata hivyo Mratibu huyo alisema kuwa kwa ujumla jamii aina budi kuungana kwa pamoja kwa lengo la kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia ambavyo vimekuwa tishio hapa nchini katika maeneo mbalimbali.

“Sisi kama waratibu wa kituo hiki tumeweza kujitoa ili kusaidia watoto hawa hivyo jamii hawana budi kuungana kwa pamoja kwa lengo la kupinga vitendo hivi vya ukatili ikiwa ni pamoja na kupinga unyanyasaji wa watoto”. alisema China.

Naye mkurugenzi wa kituo hicho Sisita  Hellena alisema kuwa aliamua kuanzisha kituo hicho kwa lengo la kuwasaidia watoto wenye mahitaji maalumu.

“Mimi hawa watoto hawa naishi nao vizuri sana japokuwa changamoto ninazo ziopata ni pamoja na serikali kusahau watu ambao tunajitoa ili kuweza kuwasaidia watoto changamoto ni kubwa sana” alisema Hellena.

Lengo la mbunge huyo kutembelea kituo hicho ni moja ya kutimiza ahadi yake ambayo aliweza kuhaidi watoto hao hivi karibuni kabla ya sikuku alipotembelea kituo hicho na kuwapelekea Mafuta ya kula, Sukari, Sabuni za kufua na kuweza kuwahaidi kuwa siku ya sikuku ataweza kushiriki chakula cha pamoja na watoto hao.

                               …….Mwisho…
Powered by Blogger.