Mbunge viti maalumu chadema atoa shilingi Millioni moja kwa waandishi wa habari
Mbunge viti maalumu chadema atoa
shilingi Millioni moja kwa waandishi wa habari
Katika
kuunga juhudi za waandishi wa habari hapa Nchini ambao wamekuwa wakifichua
maovu yanayofanywa na watumishi wa serikali pamoja na taasisisi za binafsi
Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Simiyu Gimbi Dotto Massaba ametoa shilingi
million moja fedha za kitanzania kwa lengo la kuwaunga mkono chama cha wandishi
wa habari mkoa wa simiyu Simiyu Press
Club (SMPC) kwa lengo la kununua vitendea kazi na kuboeresha ofisi yao ili ili
kuboresha ufanisi wa kazi yao.
Ni katika
ziara ya kibunge ambayo inafanyika mkoani humo kwa lengo la kuongea na wananchi, Mbunge huyo
amesema kuwa ameamua kutoa msaada huo kwa waandishi wa habari kwa kutambua
umhimu wa vyombo vya habari hapa nchini kwani vimekuwa vikifichua mambo
mbalimbali huku vikielimisha jamii.
Aidha mbunge
huyo alisema kuwa mbali na kutokuwa na mfuko wa jimbo ameam ua kutoa msaada huo
wa fedha kwa lengo la kuunga juhudi za waandishi wa habari ambazo wamekuwa
wakizifanya kwa lengo la kelimisha jamii na kufichua maovu ya baadhi ya viongzi
wa kiserikali hapa nchini.
“Katika mkoa
huu wa simiyu natambua umhimu wa vyombo vya habari kwa moyo wangu wa dhati
kutoka katika mshagara wangu nawachangia shilingi laki moja ili kuendeleaza
ofisi yenu ikiwa ni pamoja na kununua mahitaji muhimu kwa lengop la kuongeza
ufanisi katika kazi zenu alisema Gimbi.
Kwa upande
wake mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari mkoani Simiyu Frank Kasamwa
ametoa shukrani kwa niaba ya wanachama hao huku akisema kuwa v iongozi wengine
hawana budi kuunga mkono vyombo vya habari kwa lengo la kujenga mkoa wa simiyu.
Aidha
Mwenyekiti alisema kuwa moyo alionayo mbunge huyoi kwa lengo la kuwasaidia
wananchi itakua chachu kubwa katika kuleta maendeleo ndani ya mkoa.
“Wapo
viongozi wengi hawatambui umhimu wa vyombo vya habari lakini kutokana na
kutambua umhimu wa vyombo vya habari ndani ya mkoa huu tutashirikiana” alisema
Mwenyekiti.
Mbunge huyo
wa viti maalumu mkoa wa simiyu kupitia
CHADEMA Gimbi Masaba ambaye pia ni mwenyekiti wa chama cha demokrasia na
maendeleo chadema Wilayani Itilima
ameanza rasmi ziara ya kutembelea maeneo mbalimbali ikiwemo sekta ya Afya ,
Miundo mbinu ya barabara na Elimu ili kubaini changamoto mbalimbali zinazowakabili
wananchi wake huku akisema kuwa yeye ni mbunge wa wananchi wote wa mkoa wa
simiyu.
……Mwisho….