SERENGETI FC WAILAZA SONGAMBELE KICHAPO CHA BAO3-1

PICHA YA MRATIBU WA MASHINDANO YA KUPINGA VITENDO VYA UKATILI WA KIJINSIA  KUTOKA PLAN IMTERNATINAL JASTIN MAHIMBO AKIKABIDHI NGAO YA USHINDI KAPTENI WA TIMU YA SERENGETI FC BAADA YA KUILAZA KICHAPO CHA BAO3-1 SONGAMBERE FC

SERENGETI FC WAILAZA SONGAMBELE KICHAPO CHA BAO3-1

Plan International kwa kushirikiana naUmoja wa nchi za ulaya, Jukwaa la utu wa mtoto CDF, na Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF wameitimisha mashindano ya  mpira wa miguu iliyokuwa imeanzishwa kwa lengo la  kupinga  vitendo vya ukeketaji na ndoa  za utotoni wilayani Tarime Mkoani Mara.

Katika michuano hiyo iliyofanyika kwenye viwanja vya serengeti mjini Tarime kwa kushirikisha Timu takribani sita hii mashindano hayo yameitimishewa jana huku Serengeti fc wakiilaza songambele fc kichapo cha bao3-1.

Kipindi cha kwanza serengeti waliweza kuchungulia nyavu za songambele mabao Matatu  mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika serengeti walikuwa wanaongoza bao tatu nunge.

Ndipo kipindi cha pili Dk ya 51 Songambele waliweza kupata bao la kufutia machozi  kupitia kwa mchezaji mwenye jenzi namabri sita mgongoni  Elia Nicholas.

Timu ya serengeti bao lilipachikwa dk 03 kupitia kwake Abdalah Hamis kmupitia kona na Bao la pili Dk 06 kupitia kwakeZachalia Maliki huku bao la Tatu likichikwa naye Daudi Daud 26 kipindiocha kwanza, mpka kipindi cha kwanza kinamalizika Serengeti walikuwqa wanaongoza kwa bao 3-0.

Jastin Maimbo kutoka Shirika la Plan Internatinal ambaye pia alikuwa Mratibu wa mashindano alisema kuwa yameanzishwa mashindano hayo kwa lengo la kupinga vitendo vya Ukeketaji, Ndoa za Utotoni pamoja na Mimba za utotoni Wilayani Tarime Mkoani Mara.

Tunajua vijana waliowengi bada hawajaoa na pia vijana wanapenda michezo hivyo kupitia Michezo jamii itaweza kupata Elimu na timu zinazoshiriki ni sita lakini kadili michezo inavyoendelea lazima timu zitaweza kuongezeka kwa ni mradi huu ni wa takribani miaka miwili alisema Maimmbo.

Kwa upande wake Makamu mwenyekiti wa chama cha mpira wilayani Tarime Mkoani Mara TAFA Gweso Nyakisagane alisema kuwa jamii haina budi kuondokana na masuala mazima ya vitendo vya ukeketaji na kuzidi kuboresha suala zaima la Michezo.

Timu zilizokuwa zinashiriki mashindano ni timu sita ambazo ni Serengeti FC,Nyamwaga Fc, Ngerengere FC, Susuni Fc, Songambele Fc na Sirari Fc.

Mshindi wa kwanza aliibuka Serengeti Fc baada ya kuilaza Songambele kichapo cha bao3-1 na kuweza kujinyakulia Ngao ya Ushindi pamoja na Boksi mbili za soda huku Mratibu wa mashindano hayo kutoka plan International Jastin Mahimbo akidaia kuwa mashindano yajayo lazima wataandaa zawadi kubwa kwqa ajili ya kutoa hamasa kubwa.
........Mwisho...

Powered by Blogger.