CDF WAZINDUA FILAMU YA KUPINGA VITENDO VYA UAKATILI.

PICHA YA MKUU WA WILAYA YA TARIME GLORIUS LUOGA AKIONGEA NA WSHIRIKI WA KATIKA UZINDUZI WA FILAMU YA GHATI NA RHOBI

              CDF WAZINDUA FILAMU YA KUPINGA VITENDO VYA UAKATILI.
Shirika lisilokuwa la kiserikali jukwaa la utu wa Mtoto CDF wamezindua filamu ya simulizi halisi ya   Ghati na Rhobi kwa lengo la kufikisha ujumbe kwa jamii ili kuweza kuondokana na mila potofu zilizopitwa na wakati ikiwemo Ukeketaji.

Filamu hiyo ya simulizi halisi iliyoyumia picha ya katuni katika kufikisha ujumbe kwa jamii imezinduliwa rasmi jana na mkuu wa wilaya ya Tarime Glorius Luoga katika ukumbi wa Sky Hotel

Filamu  ya Ghati na Rhobi ni hadithi inayohusu wasichana wawili wanaopinga ukeketaji katika jamii yao wasichana hao wameonesha ujasili kwa kukataa kitendo hicho chenye maumivumakali  na filamu hiyo imeonesha kuwa siyo  jamii zote hapa Tanzania zinajiusisha na suala zima la ukeketaji na kwamba maeneo mengi wameamua kuondokana na mila hizo potofu na kuungana pamoja ili kuweza kupinga vitendo hivyo.

Akizindua filamu hiyo Mkuu wa Wilaya ya Tari ne Glorius Luoga ameitaka Jamii kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia ikiwemo ndoa za utotoni Mimba za utotoni pamoja na ukeketaji kwa lengo la kumkomboa mtoto wa kike ili aweze kutimiza ndoto yake ikiwemu Elimu  huku walimu wa shule za misingi na sekondari wajikite kutoa Elimu juu ya madhala ya Ukeketaji ili kuweza kupunguza vitendo vya ukatili dhidi ya mtoto wa kike.

Mkuu wa wilala huyo alisema  kuwa jamii kwa ujumla kupitia taasisi za serikali na zisizokuwa za kiserikali hawana budi  kuungana kwa pamoja ili kuweza kutokomeza mila potofu zilizopitwa na wakati ambazo zimekuwa zikimukandamiza mama na mtoto

"Tufike wakatia suala hili tulitokomeze sisi wenye siyo kila mwaka mashirika yanaimba masuala ya ukeketaji Ndoa za utotoni na Mimba za utotoni na jamii ya kikurya hamtaki kubadilika pia ni jukumu la walimu wa shule z misingi na sekondari kuendelea kutoa Elimu hii hata mashuleni" alisema Mkuu wa Wilaya.


Margaret sawe Massai ni Kaimu mkurugenzi maendeleo ya watoto katika wizara ya maendeleo ya jamii jinsia na watoto amesema kuwa mtoto wa kike anastahili  kulindwa ikiwa ni pamoja na kupata haki zake za msingihivyo kama vile Elimu na makuzi bora hivyo  kama serikali wanazidi kupinga vitendo hivyo vya ukatili dhidi ya mtoto wa kike huku akitaka jamii ambayo bado inakumbatia mila potofu kuondokana nazo ili mtoto wa kike aweze kupata haki yake ya msingi.

Kwa Upande wake Spihia Temba kutoka shirika la CDF ambao ni waandaaji wa filamu hiyo kwa kushilikiana na Shirika la Forward katika kueleza lengo la uzinduzi wa filamu hiyo ya Rhobi na Ghati alisema  kuwa filamu hiyo imezinduliwa kwa kipindi hiki kwani baadhi ya koo za wakurya wilayani Tarime Mkoani Mara wataanza kukeketa mtoto wa kike hivyo kama shirika ambao pia ni wadau wa kupinga vitendo hivyo vya ukatili wameona kutoa elimu mapema ili jamii hiyo iweze kuondokana na mila potofu ususani ukeketaji.

Mbali na kuzinduliwa rasmi kwa filamu hiyo Sophia aliongeza kuwa pia watazunguka takribani shule za msingi kumi na tano huku wakitoa  Elimu kupitia filamu hiyo pamoja na Masoko na meneo yenye mikusanyika ya watu lengo ni kufikia jamii nzima ili kuweza kubadili mitazamo hasi.

Katika uzinduzi huo wa filamu wameweza kushirika wazee wa Mila, Afisa maendeleo ya jamii, Walimu wa shule za Msingi na Sekondari, Viongozi wa Dini, Wanafunzi wa shule za misingi watendaji wa vijiji na kata  huku viongozi wa dini wakiahidi kuendelea kueneza ujumbe kwa waumini wao ili kuondokana na mila potofu huku wakimwogopa mwenyezi Mungu.

 Mchungaji Thobia Ruochi ni mwenyekiti wa makanisa ya Wapentekoste alisema kuwa viongozi wote wa dini zote hawana budi kufundisha madhara yanayotokana na ukeketaji huku jamii ikimurudia mwenyezi mungu na kufuata yale wataalamu wanayofundisha katika semina mbalimbali na Kongamano.

"Sisi viongozi wa dini ni jukumu letu kuhubiri mazuri kulingana na bibilia inavyosema lakini bibulia haijatoa maagizo kuusu binti kukeketwa hivyo waumini na wakristo wote wanaenda kinyume na Mwenyezi Mungu hawana budi kubadilika" alisema Ruochi.
.....Mwisho.....

Powered by Blogger.