LOWASSA ATANGAZA NEEMA KWA WAKULIMA.
LOWASSA ATANGAZA NEEMA KWA WAKULIMA.
Mgombea Urais kupitia kupitia Umoja wa katiba ya Wananchi UKAWA chini ya mwamvuli wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Edward Lowassa amesema kuwa endapo atachaguliwa atatoa kipaumbele katika suala zima la kilimo ili kuweza kuwakomboa wakulima kwani asilimia kubwa kipato cha Taifa kinatokana na Kilimo.
Aidha Mgombea huyo alisema kuwa Wakulima wamesaulika pasipokuwepo sababu za msingi ikiwa ni pamoja na kuzuiwa kupeleka mazao yao Nje ya Nchi kwa lengo la kutafuta masoko ili kuweza kujikomboa kiuchumi na kuongeza pato la Taifa.
"Nikiwa rais lazima wakulima waweze kuuza mazao yao Nje ya Nchi mipaka inayowekwa na jeshi la polisi lazima itolewe ili kila mkulima aweze kuwa na uhuru wa kuuza Nje ya Nchi mfano nyie wakulima wa Tarime mtakuwa na haki ya kuuza mazao yennu Nchi jirani ya Kenya lengo ni kufukuaza Umaskini Mwenye kuku Ishirini awe na Arobaini" alisema Lowassa.
Hayo yamebainishwa jana katika viwanjia vya Serengeti Mjini Tarime kipindi akiongea na wananchi katika mkutano wa hadhara kwa lengo la kunadi sera zake pamoja na kuwanadi wagombea Udiwani akiwemo Mgombea Ubunge jimbo la Tarime Mjini Esther Matiko pamoja na Mgombea Ubunge jimbo la Tarime Vijijini John Heche kupitia Chadema.
Kwa upande wake Mgombea Ubunge Jimbo laTarime Mjini kupitia Chadema Esther Matiko akitaja changamoto zinazowakumba wanatarime mbele ya Mgombea Urais kupitia chadema Edward Lowassa alisema kubwa Tarime inakumbwa na tatizo la ukosefu wa Maji hivyo amemwomba mgombea urais kuwa endapo atachaguliwa wananchi wapate maji safi na salama yanayotokana na Ziwa Victoria
Hata Hivyo Matiko aliongeza kuwa kuhusu suala la Elimu ambalo CHADEMA wamesema kuwa ndo kipaumbele cha kwanza bado wanafunzi wa Shule za Msingi Mfano Azimio, Mapinduzi, Sabasaba, Nyamisangura na Rebu bado wanasoma kwa zamu inamaana wanapishana suala ambalo linaweza kupelekea kushuka kwa taaluma hivyo amemwomba Mgombea Urais kufanyia kazi suala hilo endapo atapewa ridhaa na wananchi ikiwa ni pamoja na kupandisha madaraja ya Walimu huku wakiongezewa mishahara na kulipwa kwa wakati.
Naye Mgombea Ubunge Jimbo la Tarime Vijijini John Heche alisema kuwa atahakikisha wananchi wa Nyamongo wana lipwa foidia zao mara moja baada ya Kuchaguliwa kuwa Mbunge wa Tarime vijijini.
Suala la fidia limepigiwa kelele kwa muda wa kutosha sasa suluisho la Tatizo hilo ni kuhakikisha wananchi munakipa ridhaa chama cha Upinzani ili mimi kwa Kushirikiana na Mbunge wa Tarime Mjini na Rais anyetokana na UKAWA tunatatua matatizo ya Wanatarime mara moja.
Mgombea Urais huyo ametokea Wilayani Serengeti na kuweza kuongea na wakazi wa Nyamongo na badae kuelea Mji Mdogo wa Sirari na kurejea Tarime Mjini katika Viwanja vya Serengeti huku akidai kuwa Lengo lake ni kutokomeza Umaskini.
Mwisho.....