JAMII YATAKIWA KUKEMEA VITENDO VYA UKATILI WA KIJINSIA TARIME.
PICHA YA MKURUGENZI WA SHIRIKA LA TARIME MINDSET NETWORK CLEOPHACE SABURE AKIONGEA NA WANAFUNZI KATIKA SHEREHE ZA MAADHIMISHO YA SIKU YA MTOTO WA KIKE DUNIANI. |
kulingana na Takwimu za mwaka 2010 Imebainika kuwa kwa wastani wa wasichana wawili wili kati ya watano wanaolewa kabla ya umri wa miaka kumi na nane huku mamailioni ya wasichana wakiolewa kabla ya kufikia umri wa kubalehe Ambapo Nchi 31 kati ya 41 Duniani ndoa za utotoni ni asilimia 30 ambapo zinapatikana Nchi za bara la Afrika.
Hayo yamebainishwa Jana na na Mkurugenzi wa shirika la Tarime Mind Set Network Cleophace Sabaure katika Sherehe za Siku ya Mtoto wa kike Duniani ambzo uadhimishwaa Tarehe 11 October kila mwaka huku maadhimisho hayo yakiambatana na sherehe mbalimbali ili jamii ikipate Elimu kupitia Kongamano hizo.
Shirika la Tarime Mindset Network(TMN) wamefanya maadhimisho hayo jana katika viwanja vya shule ya Msingi Turwa kwa kushirikisha wanafunzi wa shule za Misingi pamoja na Wanafunzi ambao wako kwenye klabu za kupinga Ukatili wa kijinsia kutoka kila shule zikiwemo shule za sekondari, kwa lengo la kuadhimisha siku ya mtoto wa kike duniani huku wakiwa na kauli mbiu isemayo kuwa badilisha fikra acha ukatili wa kijinsia.
Mkurugenzi wa Tarime Mind Set Network Cleophace Sabure ametaja mikoa inayoongoza kwa ndoa za utotoni kuwa ni pamoja na Shinyanga 59%Tabora58 %Mara 55%Dodoma 51% Lindi 48% Mbeya 45%Morogoro 42%Singida 42%Rukwa 40%Ruvuama39%Mwanza37%Kagera 36%Mtwara 35%Manyara 34%Pwani 33%Tanga29%Arusha 27%Kirimanjaro27%Kigoma 26%Dar ers salaam 19% na Iringa mkoa wa Mwisho 08%. kutokana na takwimu zilizochukuliwa mwaka 2010 huku akizidi kutoa mwito kwa jamii hkuondokana na Suala zima la ukatili wa kijinsia ikiwemo Ukeketaji
"Hakuna haja ya kuendelea kuamini mila potofu ambazo zimepitwa na wakati jamii tushikamane kwa pamoja ili kuweza kupinga Vitendo hivyo vya Ukatili" alisema Cleophace.
Ameomgeza kuwa duniani kote mwanamke mmoja kati ya watatu anakumbana na ukatili wa kijinsia katika maisha yake huku zaaidi ya wananwake millioni 700 walioko hai duniania waliolewa kabla hawajafikisha umri stahiki wa kuolewa na kudai kuwa bila hatua za pamoja idadi itaongezeka na kufikia zaidi ya billioni 1.2 ifikapo mwaka 2050 jambo ambalo mashirika kwa kushirikiana na sereikali hawana budi kukememea mambo hayo ili kuweza kumkomboa mtoto wa kike .
Kwa Upande wake Mwl William Makusanyo ambaye alikuwa mgeni Rasmi katika maadhimisho hayo alisema kuwa kuwa watoto wa shule za misingi ni majeshi ya ukombozi hivyo watakuwa chachu ya mabadiliko katika kupinga vitendo hivyo vya ukatili wa kijinsia dhidi ya mtoto wa kike.
Alisema kuwa kupitia klabu mbalimbali ambazo zimeundwa katika shule za misingi ili kuweza kupinga vitendo vya ukatili klabu hizo zitakuwa chachu ya maendeleo katika kupinga fikra potofu na kuweza kupunguza vitendo vya ukatili huku mabinti wakizidi kupinga Ukeketaji pale wanaposhawishiwa na wazazi
Adella Risa Andreal kutokashule ya msingi Ronsoti ni muhitimu wadarasa la saba katika shule ya msingi Ronsoti pamoja na Jostina Josepha Darasa la sita shule ya Msingi Mapinduzi wamewasihi waschana kutokubali suala zima la kukeketwa huku mashirika yakizidi kupinga vitendo hivyo ili kumkomboa mtoto wa kike.
Naye mwenyekiti wa ATFGM kutoka Masanga alisema kuwa nia yao ni kuahakikisha mwanamke anapata haki zake za msingi na kuondokana na unyanyasaji ambao amekuwa akipata aidha kwa kufanyia vitendo vya ukatili wa kisaikorojia.
Hata hivyo Mratibu wa Ushirika Youth MindsetNetwork Thomas Muruga aliongeza kuwa lengo la mshirika hayo ni kupiga vita vitendo vya ukatili wa kijinsia ikiwemo utoaji wa Elimu kwa jamii ili kuondokana na kuamini mila potofu ambazo zimepitwa na wakati.
......Mwisho...