ASKOFU WA JESHI LA WOKOVU DUNIANI ASISITIZA UPENDO AMANI NA MSHIKAMANO.
ASKOFU WA JESHI LA WOKOVU DUNIANI ASISITIZA UPENDO AMANI NA MSHIKAMANO.
Waumini wa kanisa la jeshi la wokovu wametakiwa kudumisha umoja upendo na mshikamano ikiwa ni pamoja nakutii ujumbe wa Bwanayesukristo kuhusu wokovu kwa watu wote kwani wasipofanya hivyo kristo hataona ujumbe huo ukileta mabadiliko kwa waumini.
Kauli hiyo imetolewa na Askofu mkuu wa kanisa la Jeshi la Wokovu duniani Andr'e Cox kipindi akiongea kwenye kongamano la na wamini wa kanisa la jeshi la wokovu mikoa ya kanda ya ziwa na kati ikiwemo na Tabora katika ukumbi wa CMG wilayani Tarime Mkoani. Mara.
Askovu huyo amesema kuwa kipindi Bwana yesu kristo anakuja duniani aliweza kuacha ujumbe mwingi wenye kubadili mioyo na mitazamo ya waumini hivyo waumini hao hawana budi kufanyia kazi ujumbe huo huku wakidumisha Amani Upendo na Mshikamono.
Hata hivyo Askofu huyo alisema kuwa waumini wote hawana budi kuvaa mavazi yanayostahili ikiwa ni pamoja na kubadili mioyo yao kwa lengo la kumupendezeshea mwenyezi Mungu.
"Kulingana na tamaduni za kiafrika kwenye harusi watu wanatumia ghalama kubwa kushona nguo stahiki lakini katika madhaabu ya ya kumutukuza mwenyezi Mungu waumini hawavai nguo stahiki hivyo ni vyema kueshimu mahali pa mwenyezi Mungu" alisema Andr'e Cox
Kwa upande wake Askofu mkuu kanisa la wokovu jimbo la Tarime Willison Mwalukan alisema kuwa ujio wa kiongozi huyo wa kitaifa ni kuahakikisha anatembelea makanisa yote ya Jeshi la Wokovu kwa lengo la kufikisha ujumbe kwa waumini wote kuwa na upendo Amani na Mshikamano ikiwa ni pamoja na kufanya matendo yenye kumutukuza mwenyezi Mungu.
Hata hivyo Askofu huyo alisema kuwa wanatumia fursa hiyo kuombea Nchi kuwa na Amani katika harakati za kuelekea kwenye uchaguzi mkuu ambao upo hap mbeleni ili uweze kufanyika kwa Amani.
katika kongamano hilo zaidi ya waumini 200 wamefikia mwisho wa mafundisho ya jeshi la wokovu huku wakitakiwa kuwa askali wa kiroho na kimwili kwa lengo la kumupendezesha Mwenyezi Mungu.
...........................Mwisho.....