ACT Wazalendo wanasema kunaitajika viongozi waadilifu.

PICHA YA MGOMBEA URAIS KUPITIA ACT WAZALENDO ANNA MGHWIRA AKIONGEA NA WANANCHI WA TARIME HII KATIKA MKUTANO WA HADHARA.  
ACT Wazalendo wanasema kunaitajika viongozi waadilifu.

Chama cha ACT Wazalendo kimesema kunaitajika viongozi wenye uadilifu utu na uza lendo kwa lengo la kuitumikia Taifa ipasavyo kwa lengo la kuwaletea wananchi maendeleo ya ya haraka ikiwa ni pamoja na kufanya mapinduzi ya kweli pasipokuwepo vitisho vya aina yeyote kwani kiongozi anachaguliwa na wananchi.
Kauli hiyo imetolewa jana Mgombea Urais kupitia chama cha ACT Wazalendo Anna  Mghwira ni katika mkutano wa hadhara uliofanyika  kwenye viwanja vya shamba la bibi Serengeti Mjini Tarime .

Mgombea urais huyo alisema viongozi ambao wamekuwa wakichaguliwa na wengine kupewa wadhifa wamekuwa wakienda kinyume na taratibu za uongozi kupitia Act wazalendo kulingana na sera yao viongozi ambao wanapaswa kuchaguliwa ni wale wenye Utu Uzalendo kwa watanzania Wote bila kubgua Dini wala kabila.

Anna alisema kuwa kwa sasa watanzania wanapaswa viongozi watakao simamia rasilimalizote za nchi huku zikitumika kuwanufaisha watanzania wote.

Hata hivyo Mgombea huyo ameiomba Tume ya Uchaguzi NEC Kusimamia kura kwa kufuata kanuni na misingi yake huku wagombea wote wakichagua mawakala waaminifu wenye kuitakia Nchi Mema ili uchaguzi uweze kufanyika kwa uhuru na haki.

"Naomba vyama vyote vya upinzani tuweze kuungana pamoja na kuweza kufanya mabadiliko ya kweli lengo letu ni kutoa Chama cha mapinduzi madarakani kwani ikiwezekana nao wake nje kwa miaka Hamsini" alisema Mgombea huyo.
Kwa Upande wake mgombea Ubunge kupitia ACT Wazalendo Deogratias Meck alisema kuwa Lengo lake ni kuwakomboa vijana , Akina Mama na Wazee kuhakikisha wanapata hakiz zao za msingi.'

Hata hivyo Meck alisema kuwa endapo wananchi watampa ridhaa ya kuongoza jimbo la Tarime mjinini athakikisha analeta Viwanda vidogovidogo ili kuweza kuzalisha ajili kwa vijana ili waweze kuondokana naUmaskini ambao wamekuwa wakilia kila siku.

"Nitahakikisha ninatoa asilimia sitini ya Mshara wa ubunge nichukue mkopo wa Millioni miambili arobaini nitendeneze Saccos ya millioni 30 kila kata ili wananchi waweze kujikwamua kimaisha lengo nikuweza kuwakomboa wananchi na lazima tutaweza hilo" alisema Deogratias.

Kwa upande wake mgombea mwenza ngazi ya Urais kupitia chama hicho Hamad Yusuph amesema kuwa Tarime kunaitajika kiongozi jasiri ambaye ataweza kuvaa viatu vya aliyewahi kuwa mbunge wa jimbo la Tarime Hayati  Chacha Wangwe.
.                                                            .......Mwisho....
Powered by Blogger.