watoto zaidi ya laki moja kufanyiwa tathimini katika kusoma na kuandika.
Picha ya washiriki wa semina hiyo wakiwa makini wanamsikiliza mseminishaji |
Zaidi ya watoto laki moja kuanzia umri wa miaka 7 mpaka 16 katika shule za misingi hapa nchini wanatarajiwa kufanyiwa tathimini ili kuwatambua ulewa waokatika masomo ikiwemo kusoma Kingereza, Kiswahili na kufanya Hesabu ikiwa pamoja na kutembelea kaya na kupina Afya za watoto wenye utapia mlo kuanzia miezi 6 mpaka miaka 14 pamoja na Madini joto.
Hayo yalibainishwa na na mratibu wa UWEZO Wilayani Tarime Mkoani Mara Edward Muremwa katika Semina ya Mafunzo katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime kwa wahojaji wakiwemo Wazazi na walimu kwa lengo la kufanya tathimini katika shule za misingi ili kutambua uelewa wa wanafunzi hao kuanzia miaka 6 mpaka 14 huku wakitembelea Kaya kwa lengo la kupima madini joto na utapia mlo kwa watoto kuanzia Miezi 6 mpaka miaka 14.
"Hapa tunawafundisha hawa wahojaji 60 katika mafunzo na badae tutweza kwenda katika shule za misingi kutambua uelewa katika kusoma kusoma na kuandika kiswahili, kingereza na kufanya Hesabu na badae tutaenda katika vijiji na mitaa kwa lengo la kutembelea kaya tukipima madini joto pamoja na utapia mlo kwa watoto kuanzia miezi sita mpaka miaka 14" alisema Muremwa.
Mratibu huyo amesema kuwa zoezi hilo linafanyika nchi nzima huku wilaya 159 zikitarajia kuanza zoezi hilo ikiwa ni juhudi za katika nchi za Afrika Mashariki Kenya Uganda na Tanzania, kwa lengo la kujua uelewa wa wanafunzi katika kujua kusoma na kuandika
Akifungua Mafunzo hayo mgeni rasmi Afisa Elimu Msingi wilayani Tarime Enock Waitara alisema kuwa ufatiti huo umekuja kwa muda mwafaka ukilinganisha na Ufaulu wa darasa la saba mwaka jana mkoa wa Mara haukuridhisha hivyo kupitia fursa hiyo iatatoa hali halisi ya ufundishaji.
"Ninachowaomba mukienda katika tafiti jaribu kuleta matokeo halisi ili tuweze kuona tuko wapi kwa lengo la kujtambua na kufanya kazi ipasavyo" alisema.
Joseph Magabe ni Mwenyekiti wa Shirika la Maendeleo Tarime SHIMATA alisema kuwa mradi huo ambao unatolewa na UWEZO na kuratibiwa na shirika la Maendeleo Tarime SHIMATA wanatarajia kupima kiwango cha kusoma na kuandika kupitaia sera ya serikali ili kuweza kupatikana kwa matokeo makubwa sasa huku wakibaini changamoto na kuzifanyia kazi kwa lengo la kuboresha taaluma katika shule za Misingi.
"SHIMATA sisi ndo tunaratibu zoezi zima lakini lengo kubwa ni kuahakikisha sera ya srikali kupitia matokeo makubwa sasa inafanikiwa" alisema Magabe.
Hata hivyo washiriki wa mafunzo hayo walisema kuwa wataweza kufanya kazi kwa weredi huku wakibaini changamoto zinzowakabili wanafunzi wa shule za misingi ili ziweze kufanyiwa kazi kwa lengo la kuboresha Elimu.
..........Mwisho.....