Mgombea ubunge jimbo la Tarime mjini CCM siungi mkono mgombea Urais kupitia CHADEMA wala UKAWA.



Mgombea ubunge jimbo la Tarime kupitia tiketi ya chama cha Mapinduzi( CCM) Michael Kembaki amesemakuwa yeye ni mwanachama wa chama cha mapinduzi yeye haungi  mkono Mugombea urais kupitia Chadema Edward Lowassa kulingana na habari ambazo zimekuwa zikisamabazwa na maadui wake wa kisiasa huku nyingine zikichapishwa katika magazeti kwa lengo la kumuchafua.


Kauli hiyo imetolewa hivi karibuni kipindi akiongea na waandishi wa habari wilayani hapa baada ya baadhi ya vyombo vya habari kuandika kuwa mgombea ubunge jimbo la Tarime mjini kupitia CCM Michael Kembaki anaunga mkono mgombea urais kuptitia tiketi ya CHADEMA Edward Lowassa kuwa habari hizo ni za uongo yupo kwa ajili ya kufanya kazi za chama chae na kwa lengo la kuwaletea wananchi Maendeleo.

Akiongea na waandishi wa habari mgombea huyo alisema kuwa yeye anatumikia chama chake kuhusu habari za kuunga mkono upinzani hizo ni habari za uzushi kwa lengo la kumuchafua ili aweze kukosa imani kwa wananchi na kumpunguzia kura zake.

Aidha Mgombea huyo alisema kuwa yeye anaunga mkono Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Pombe John Magufuli na wagombea wote kuanzia Ngazi ya Madiwani na ubunge kupitia chama chake.
"Najua hao ni wabaya wangu katika mambo ya kisiasa mimi sijaongea na waandishi wa habari kuhusu kumuunga mkono lowassa hizo ni habari za uongo lazima mwandishi wa gazeti la Nipashe  la Tarehe 27 Septemba mwaka huu ukurasio wa Kumi na tano huku kichwa cha habari kikisema kuwa mgombea ubunge jimbo la Tarime amuunga mkono mgombea urais kupitia UKAWA huku ndani wakinitaja mimi na mhariri wake laziama niwachiukuliea hatua kali kwa kupotosha umma" alisema Kembaki.

Aidha Michael Kembaki aliongeza kuwa  kuwa yule mwenye mapenzi mema na Watanzania lazima ashirikiane na Chama cha Mapinduzi kwa lengo la kuwaletea wananchi maendeleo na siyo kujipanga kwa lengo la kupotosha Umma lazima wagombea wote tupingane kwa haoja na siyo kupotosha wapiga kura wetu.

Hata hivyo kembaki amesema kuwa waandishi wa habari waondokane na kutumiwa vibaya na wagombea bali wasimamaie ukweli ulivyo kulingana na Maadili yao ya habari

.......Mwisho.....
Powered by Blogger.