WATOTO WATATU WATEKETEA KWA MOTO NA KUFARIKI DUNIA RORYA.

Picha ya mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilayani Rorya Mkoani Mara wa pili kutoka kushoto akikabidhi msaada wa chakula na Godoro kwa Babu wa marehemu katikati. 
WATOTO WATATU WATEKETEA KWA MOTO NA KUFARIKI DUNIA RORYA.
Watoto watatu  katika kitongoji cha machawa kijiji cha  malonga kata ya milale Wilayani Rorya Mkoani Mara wakiwemo wawili  wa familia moja wameteketea kwa moto na kufariki dunia

Watoto hao  waliongua ni  Baraka godfrey miaka  3  Happy Idd miaka 3 ambaye ni mtoto wa dada yake na mama wa marehemu  wa  watoto hao waili   ambaye ni Baraka Godfrey na Bella Godfrey Mwenye  umri wa mwaka mmoja na Nusu.
 Elisha Muga ni Mkukazi wa kijini hapo pia ni shuhuda wa tukio hilo alisema kuwa tukio hilo lilitokea majira ya sa kumi na mbili alufajiri ni baada ya Mama yao mzazi watoto hao kuamka asubuhi kwenda kununua mboga katika mto Jirani milale  na baadae ndo waliona moto kama majirani na kufika pale kwa ajili ya msaada walikuta tayari watoto hao wakiwa wameteketea na baada ya moto kuisha waliweza kutoa marehemmu hao na kuwaifadhi kwenye jiko.

"Watoto wa marehemu walikuwa wawili mtoto wa umri wa ,miaka mitatu na mmoja na Nusu na mwingine alikuwa mtito wa dada yake Mama wa marehe alikuwa amekuja kuwatembelea" alisema Elisha.

Guka Nyapala ni Babu wa watoto hao ambao wameteketea kwa moto alisema kuwa alipoamka majira ya asubuhi aliweza kuongea na simu na mama wa marehemu nakwambiwa kuwa watoto wamelala salama na badae alishangaa kupigiwa simu kuhusu kuteketea kwa moto watoto hao.
"Nimeamka mapema nikaja kufunga Mifugo yangu hapa karibu na nyumba nilipoona mlango umefungwa badae nikaenga kumwona fundi wangu anayenichania mbao na ndiyo badae nilipigiwa simu kuhusiana na tukio hilo" alisema Babu wa watoto hao.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilayani Rorya Mkoani Mara Samwel Kiboye baada ya kuguswa na tukio hilo ametoa msaada wa Godoro moja, Blanketi, Mashuka, Nguo, Kilo Miamoja za mchele, Mafuta ya kupikia, Sabuni na  Chumvi na shilingi laki moja huku akisema kuwa viongozi wa chama hicho watajipanga kwa ajili ya kumujengea makazi mapya.

"Hili tukio limetugusa wote watanzania na sisi kama chama tumeamua kuwasadia wananchi hawa kwa sababu nyumba yao imeungua na vitu vyote vimeungua ndani na alikuwa na watoto wawili wote wameteketea ndani ya nyumba" alisema Samwel.
Chanzo cha tukio hilo hakijafaamika
Powered by Blogger.