Picha ya Mwenyekiti Chama cha Mapinduzi wilayani Rorya Mkoani Mara Samwel Kiboye akiongea na makatibu ho leo katika ukumbi wa chama Wilaya kujusiana na uchaguzi utkaofanyika Mosi Mwaka huu kwa lengo lakumpta atakayepeperusha bendera ya chama hicho.

Picha ya Mwenyekiti Chama cha Mapinduzi  wilayani Rorya Mkoani Mara Samwel Kiboye akiongea na makatibu ho leo katika  ukumbi wa chama Wilaya  kujusiana na uchaguzi utkaofanyika Mosi Mwaka huu kwa lengo lakumpta atakayepeperusha bendera ya chama hicho.
                                                         Rorya.
Mwenyekiti CCM Rorya awataka makatibu wa kata na Tawi kuwa na mshikamano.
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi wilayani Rorya mkoani Mara Smwel Kiboye amewataka Makatibu wa Kata na Matawi kuzidi kudumisha Umoja ikiwa ni pamoja na kuondokana na upambe kwa wagombea wanaowania kiti cha ubunge  na udiwani wilayani umo kwa lengo la kupata kiongozi aliyebora atakaye weza  kuleta mabadiliko.
Kauli hiyo imetolewa leo katika kikao kilichowakutanisha makatibu Tawi na Wenyeviti wa matawi kwa lengo la kupewa maelekezo juu ya uchaguzi uliopo mbeleni katika kura za maoni  kwa lengo la kumpata kiongozi mmoja atakaye peperusha bendera  ya chama hicho kuptia kura za maoni zitazofanyika hivi karibuni.
Mwenyekiti alisema kuwa makatibu wa kata waondokane na ushabiki ikiwa ni pamoja na kushawishi wanachama kupiga kura kwa wapambe wao bali waondokane na ushawishi huo ili wananchama hao waweze kufanya maamuzi sahihi bali waondokane na ushawishi huo unaweza kuwapelekea kuchaguliwa viongozi waovu kwa sababu ya kununuliwa.
Samweli aliongeza kuwa watendaji wote wa chama hicho waondokane na kutumiwa vibaya na baadhi ya wagombea ambao wanauchu wa madaraka nia yao ni mbaya kwa wananchi kiongozi mwenye nia nzuri na wananchi hawezi kuwa na makundi yeyote ambayo yanasababisha kugawanya wananchi.
"Makatibu tawi wengine wamegeuka kuwa makampena wakubwa huku wakitukana watu suala ambalo ni kinyume cha sheria uongozi ni dhamana naomba tuweke chama mbele watu badae chama chetu kikianguka tutaogopa kuja hata hapa tulipo kwa sasa" alisema Samwel.
"Nimepta malalamiko kata ishirini pia wagombea udiwani wamaegawanya watu kwa sababu ya kuwapa fedha ndogondogo suala ambalo linazidi kuchafua chama hebu nyie matatibu tawi nendeni mkae pamoja muweze kuwa na nguvu moja kwa lengo la kuvusha chama cha mapinduzi ambacho kiko madarakani" alisema Mwenyekiti.
"Makatibu tawi wanamgombea wao, Katibu tawi anamgombea wake mhazini namgombea wake suala ambalo ni baya sana "alisema Samwel.

Hata hivyo mwenyekiti huyo alikemea kitendo cha  katibu Tawi la Buganjo kata ya Bukwe kwa kitendo alichofanya kukata majina ya wananchama70 waliohai na kuweka wanachama wabovu hivyo amesimamishwa kazi kwa kukosa sifa ya uongozi baada ya kufanya kitendo hicho 

Sanjari na hayo Mwenyekiti huo aliweza kuwasomea wajumbe wa kikao hicho kanuni za uchaguzi wa CCM  huku akiwasihii kufuata kanuni hizo kwa lengo la kulinda chama na ili kizidi kuaminiwa na watanzania.

                                                                       
Powered by Blogger.