Mwenyekiti UWT Rorya ahamia CHADEMA.

Aliyesimama kushoto Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake CCMWilayani Rorya mkoani Mara ambaye pia ni Diwani wa Viti maalumu Pendo Odele akikabidhiwa kadi na Katibu wa Chadema Wilayani Rorya  Akechi Otuoma  wa tatu kulia, mbele ya wajumbe wa kamati tendaji ya chama kadi no. 2657476 .
Mwenyekiti UWT Rorya  ahamia CHADEMA.
Mwenyekiti wa umoja wa akina mama wilaya ya Rorya mkoani mara Bi Pendo Bernad Odele ambaye pia ni diwani wa viti maalumu Tarafa ya Nyancha  kupitia chama cha mapinduzi CCM  amejiuzuru wadhifa huo na kujiunga na ukawa kupitia chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) kwa kile alichodai kuwa ni kutokuwepo kwa haki na usawa katika chama  hicho ikiwa ni pamoja na kutotendewa haki na baadhi ya viongozi ngazi ya wilaya.

Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake amesema kuwa ameamua mwenyewe kujiunga na CHADEMA bila kulazimishwa na mtu yoyote  kwa lengo la kuwaletea wananchi maendele bila kujali itikadi chama chochote ikiwa ni pamoja na kuepusha migogoro iliyokuwepo baina yake na uongozi wa chama ngazi ya wilaya,
"Nimesakamwa sana na uongozi na kuandikwa na kuchafuliwa kqwenye vyombo vya habari kwa sababu zisizokuwa za msingi hvyo nimeamua kwa maamuzi yangu kuhama chama cha mapinduzi na kujiunga na UKawa kupitia CHADEMA" alisema Pendo.
Aidha Bi Pendo alisema kuwa  ameweza kutumikia chama cha mapinduzi kwa muda mrefu lakini bado hawakutambua umhimu wake sasa amefikia hatua ya mwisho kwa lengo lakuleta mabadiliko kupitia chama cha upinzani.
Hata hivyo Mwenyekiti huyo ametoa shukrani zake za dhati kwa akina mama hao ambao walimwezesha kupata kiti hicho cha wenyekiti akiwa ndani ya CCM kwani kupitia uongozi huo aliweza kuwatumikia vyema  kwa kufuata misingi na kanuni za chama bila kubagua mtu yeyote.

Kwa upande wake Katibu wa  CHADEMA wilaya ya rorya  akech otuona amekili kumpokea mwanachama huyo huku akisema kuwa mpaka sasa wameisha pokea madiwani wawili na kuwakabidhi kadi za chama  cha Demokrasoia na maendeleo CHADEMA wanachama nakusema kuwa  chama hicho kulingana na kanuni zake kinaruhusu mwanachama kujiunga nakuomba wadhifa wowote katika uongozi ndani ya cham .
"Chama chetu cha Chadema sera yake inasema kuwa  mtu aliyeingia siku moja na yeye na haki za kugombea sawa na mwananachama aliyeingia mwaka  1992 hakina ubaguzi wowote kwahiyo na sasa bado tunaitaji wanachama wengine wa kutosha " alisema  katibu chadema Wilaya.

Hata hivyo katibu huyo alisema kuwa  lengo la chadema ni kuondoa serikali ya CCM  Madarakani na kuweza kuleta mabadiliko huku wakitetea wanyonge waliokosa haki zao za msingi ikiwemo Elimu, Afya na Maji.

"Hospitali zanakosa madawa wanafunzi wanarundikana madarasani hakuna maji lakini serikali ya CCM imekaa kimya hebu wananchi watuamini na kutukabidhi nchi ili tuweza kuwaletea maendeleo" alisema katibu.
...
 



Powered by Blogger.