12 CCM WATANGAZANIA KUGOMBEA UBUNGE TARIME WAMO DC KANGOYE,WAZIRI KABAKA,NYANGWINE NA KATIBU TARAFA.

Tarime
Watu wapatao saba kupitia Chama cha Mapinduzi(CCM) wametangaza nia ya kugombe Ubunge Jimbo la Tarime huku watu sita wakitangaza nia kugombea Ubunge Jimbo Jipya la Tarime mjini .
Katibu Mwenezi wa CCM Wilayani Tarime Sospiter Samsoni alisema kuwa watu 12 walirejesha fomu na walitimiza vigezo ambavyo vilikuwa ni kuzingatia kanuni za uchaguzi ndani ya chama.
Samsoni aliwataja wanaogombea Ubunge Jimbo la Tarime ni Christopher Kangoye ambaye ni Mkuu wa Wilaya Arusha,Nyambari Nyangwine Mbunge wa Jimbo la Tarime anayetetea jimbo,Pius Marwa,Maseke Muhono,Lucas Mwita ,Paul Matongo na Charles Machage.
Kwa jimbo jipya la Tarime mjini wanaotangaza nia ya Ubunge ni Waziri wa kazi na Ajira Gaudensia Kabaka,Maico Kembaki,Philipo Nyirabu, Jonathani Machango,Ditu Manko na Brito Burure.
Samsoni alisema kuwa watangazania wote kwa pamoja watapita kwenye Kata na matawi yake ya CCM ili kuwaomba wanachama kuwachangua mmoja miongoni mwao kuwa Mbunge zoezi litakaloanza Julai 20-30,2015 .
“Hakuna mtangazania ya Ubunge ambaye atapiga kampeni kivyake wote tutawazungusha kwa pamoja kuomba kura,lengo la kuwasambaza pamoja ni kuhepusha makundi,na kejeri baina ya mtangazania na mwenzake tunataka waseme makusudio yao kwa wananchi na siyo kutukanana”alisema Samsoni.
Mtangaza nia Christophera Kangoye alisema kuwa ameamua kutangazania ili awatumikie wananchi wa Tarime na kipaumbele chake ni kuhakikisha haki inatendeka kwa kila mtu na amani inakuwepo hivyo matarajiyo yake ni ushindi.
Charles Machage Mwenye elimu ya Shahada ya Uzamili ya uongozi na Biashara alisema kuwa iwapo atachaguliwa atahakikisha Tarime inakuwa kiuchumi kwa kile alichoeleza kuwa Tarime ni wafugaji,wakulima, wafanyabiashara na kuna Madini lakini bado uchumi uko chini.
Jonathan Machango ambaye ni Katibu Tarafa ya Inchage-Tarime alisema kuwa akiwa Mbunge atahamasisha maendeleo Tarime kwani nafasi aliyonayo ni mtawala ambayo umlazimu kutumia nguvu lakini siasa unahamasisha na sio kutumia nguvu.
Brito Burure(28) alisema kuwa akichaguliwa atahakikisha Tarime kunakuwepo na miingiliano ya watu ikiwemo kuanzishwa kwa vyuo vya elimu kwa madai kuwa kukiwepo na mwingiliano wa makabila tofauti itasaidia kupunguza ukabila ambao umesababisha migogoro ya koo kwa jamii ya Wakurya .
Kwa upande wake Mmoja kati ya watia nia hao Michael Kembaki alisema kuwa endapo atawea kupitishwa na chama chake ataweaza kuwapa kipaumbele vijana wote ikiwa ni pamoja na kuwaletea wananchi maendeleo ikiwa ni pamoja na haki na usawa kwa wote.
"Mimi ni mtu anayependa maendeleo ya wananchi wangu sitakubali kuona mwananchi ananyanyaswa nawakati nimechaguliwa kwa lengo la kuwatetea wananchi wangu" alisema Kembaki ambaye anawania jimbo la Tarime Mjini baada ta Tume ya Uchaguzi kutangaza majimbo mapya.