Matiko awaawasa boda boda kutafuta leseni na kufuata sheria za usalama barabarani.
Picha ya mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Mara CHADEMA Esther Matiko kushoto akikabidhi Tisheti Miamoja kwa Mwenyekiti wa Chama cha waendesha pikipiki Rebu Sokini kama mlezi wa Chama hicho jana katika ukumbi wa Machumbe Wilayani Tarime Mkoani.
Tarime.
Matiko awaawasa
boda boda kutafuta leseni na kufuata sheria za uisalama barabarani.
Imeelezwa kuwa Elimu ndogo
kwa Waendesha pikipiki bodaboda ni chano kikubwa kinachopeleke madereva hao kutofuata ksheria za Usalama barabarani na kuzidi kusababisha kuongezeka kwa ajiali za barbarani
hapa Nchini.
Hayo yamebainishhwa jana
katika ukumbi wa Machumbe kipindi mbunge wa viti maalumu mkoa wa Mara alipokuwa
akiongea na waendesha pikipiki hao kipindi walipo kuwa kwenye kikao cha
kujadili mienendo na tabia za waendesha pikipiki hao katika ukumbi wa Machumbe
Wilayani hapa.
Mbunge huyo alisema kuwa
waendesha boda boda hawana budi kufuata sheria za usalama barabarani kwa lengo
la kupunguza ajari za barabarani huku wakiwa na leseni kwa lengo la kuondoa
usumbufu ambao umekuwa ukijitokeza na bodaboda hao kulalamikia viongozi wa
usalama barabarani.
Aidha matiko aliongeza kuwa
ajira za bodaboda zimekuwa mkombozi mkubwa katika kupunguza uharifu ususani
maeneo ya mjini hivyo serikali haina budi kuwapa vipaumbele vijana hao ambao
tayari wameunda kikindichenye jumla ya wanachama 107 na kutambulika kwa jina la
Umoja wa Madereva Pikipiki Rebu Sokoni (UWAMAPIRESO) ambapo chama hicho mlezi
wakle ni mbunge huyo ambapojana ametoa tisheti Miamoja zenye nembo uya chama
hicho ili kuweza kutambulika vyema pale wanapobeba abiria.
“Mkiwa mmevaa tisheti hizi ni
rahisi mtu kukutambua kuwa wewe unatoka chama gani kwani hapa mjini kuna vyama
vingi vya waendesha pikipiki” alisma Mbunge.
Leonce Matto ni Mwenyekiti wa
Baraza la Vijana Chadema Iringa mjini alisema kuwa Tathnia ya waendesha
bodaboda hapa nchini imecchukua nafasi kubwa lakini bado serikali haijawapa
kipaumbele jambo ambalo ni changamoto kubwa na kusababisha vijana kuendelea
kuchukia serikali iliyopo madarakani.
uendesha
“Viongozi wa serikali wanakuja
wamekuwa wakitoa ahadi nyingi kwa vijana wakiwemo waendesha pikipiki lakini
bado hawatekelezi suala ambalo linazidi kuwakatisha tama vija wengi wa
tTanzania’ alisema Matto.
Ysuph Edward ni katibu wa
Waendesha pikipiki Katika Halmashauri ya mji wa Tarime amezidi kusema kuwa changamoto
kubwa inayowakabili ni ukosefu wa Elimu ya Usalama barabarani huku Afisa
Mahusiano Edward Mtiba amedai kuwa Viongozi wa usalama barabarani ndo kikwazo
kkikubwa kwao.
“Sisi hizi ndo ajira zetu
lakina bao jeshilapolisi linatusumbua sana limetugeuza mtaji” alisema Edward.
…..Mwisho….