Matiko achukua fomu ya kuwania jimbo la Tarime.
Picha ya mbu nge wa viti maalumu kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Mkoa wa Mara Esther Matiko akionesha fomu yake mbele ya waandishi wa habari katika ofisi ya Chama Wilayani Tarime Mkoani Mara
Matiko achukua fomu ya kuwania jimbo la Tarime.
Mbunge wa Viti maalumu
kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Mkoa wa Mara Esther Matiko amechuku fomu ya
kuwania jimbo la Wilaya ya Tarime kupitia Chadema kwa lengo la kuweza
kuwatumiakia watanzania ili kuleta Maendeleo.
Mbunge huyo aliwasili jana
katika Ofisi ya Chadema Wilaya kwa ajili ya kuchukua fomu hiyo na baadakueleakea katika mkutano wa
hadhara uliofanyika katika viwanja vya shamba la bibi nakuweza kuongea na
watanzania juu ya mustakabali wa Nchi huku akiwataka kuwa waewze kufanya
maamuzi sahihiya kuchagua kiongozi bora kulingana na matendo yake mazuri.
Mbunge huyo alisema kuwa
Kutokana na mapokezi aliyoyapokea tayari yameonesha jinsi gani wako na kiu
kiasi gani hivyo endapo chama kitaweza kumpitisha ataweza kufanya kazi ipasavyo
kwa lengo la kubadili maisha ya Wananchi ususani Wilayani Tarime.
“Leo nimepokelewa vizuri sana nimeamini kuwa mfume
dume ambao umeenesha unaenda kudhiilishwa kuwa sasa haupo kinachoitajika ni
kiongozi wakuweza kuwatetea wananchi na kuwasemea ili waweze kupata maendeleo”
alisema Esther.
Matiko atarudisha leo fomu katika ofisi za chama cha Demokrasia na
maendeleo chadema Wilaya baada ya
kuijaza na badae ataweza kuongea na Watanzania.
Kwa Upande wake katibu wa Vijana wilaya ya Iringa Mjini Reya
Mleleu alisema kuwa hiki ni kipindi cha wanawake kuonesha uwezo wao kwani
wamekuwa wakidanaganyika kwa muda mrefu na sasa wameamua kusaka maendeleo.
Moses Matiko Visiwa ambaye ni
Mwenyekiti wa Barala za vijana Chadema Wilaya ambaye pia ni Mwanasheria wa
Chama hicho Kanda ya Serengeti ambaye pia naye ni kati ya watanagazania14 ambao
tayari wametangaza kuwania jimbo la Tarime alisema kuwa kikubwa kilichomusukuma
kuwania nafasi hiyo ni kutumia fursa takayo pewa katika kusimamia rasimali za
watanzania ambazo ikiwa ni pamoja na ukwepaji wa kodi za makampuni ya kigeni
ambayo yamewekeza katika nchi ya Tanzania.
…….Mwisho…..